In Summary

• Alisema kuwa ako tayari mia kwa mia kulipia gharama zote za vipimo hivyo na kumtaka Pluto asihofu juu ya hilo.

Kibe amtaka Pluto kufanya DNA
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa redio ambaye sasa ni mwanablogu wa YouTube Andrew Kibe amemshauri mwanablogu mwenzake Thee Pluto kuhakikisha amechukua tahadhari na kufanya vipimo vya DNA ili kubaini kama kweli yeye ni baba wa mtoto wake Zoey.

Thee Pluto wikendi iliyopita alitangaza kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii kuwa pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu Felicity Shiru wamebarikiwa na mtoto wa kike waliyempa jina Zoey.

Kibe kwa upande mwingine anahisi kabisa huenda Pluto akawa amechezwa na kumtaka kuchukua hatua ya kubaini uzazi kwa kufanya DNA.

Alisema kuwa ako tayari mia kwa mia kulipia gharama zote za vipimo hivyo na kumtaka Pluto asihofu juu ya hilo.

“Ukiona Thee Pluto mwambie nitalipia DNA, asione ni kama sina hiyo pesa, naeza tafuta hiyo pesa, kama uko na shida na mtoto wako unashuku si wako mimi nitalipia DNA. Enda tengeneza mashati tao uandike nimesema Kibe atalipia DNA,” Kibe alizunguka kwa uhakika mkubwa mno.

Alisisitiza kuwa huenda Thee Pluto si baba halali kwa mtoto wake na ndio maana aliweka msimamo wake kutaka kusimamia gharama za DNA ilimradi tu apate kuwatumbua zaidi na kupata maudhui ya kucheka na kuzungumzia kwenye blogu yake ya YouTube.

“Wewe si baba halali.”

Kibe ambaye ni mwanablogu mwenye utata mwingi kwa mara kadha amekuwa akikosoa jinsi wanandoa maarufu nchini Kenya wanaonesha mahaba yao mitandao, jambo ambalo anasema ni la kujionesha wala si mapenzi ya kweli kama ambavyo wengine wanaweza dhani.

View Comments