In Summary

• Asante kwa kuendelea kuwafanya Wasafi, Waswahili, Wanawake na Bara zima la Afrika kujivunia,” Diamond aliandika.

Image: YOUTUBE// DIAMOND PLATNUMZ

Diamond Platnumz amemsherehekea msanii wa lebo yake Zuchu kwa ujumbe wa kumtia moyo huku mwanadada huyo akisherehekea kheri njema ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Diamond aliachia maneno mazuri yenye uhai tele kwa Zuchu akimtaka kutovutwa nyuma na jambo lolote kwani lengo lake kuu ni kutakiwa kuendelea kukwea ngazi hata baada ya kuteleza kidogo na kuanguka.

“Wiki hii tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa upya kwa msichana mwenye kipawa, mbunifu, upendo, kipaji na mnyenyekevu ambaye Tanzania imebarikiwa na @officialzuchu ...Asante kwa kuendelea kuwafanya Wasafi, Waswahili, Wanawake na Bara zima la Afrika kujivunia,” Diamond aliandika.

Alikumbuka kuwa msanii huyo ametoka mbali sana na pasi na kuwa na bidi yake kama ya mchwa basi angekuwa amechoka kitambo na kufa moyo katika Sanaa ya muziki ambayo anaitaja kama iliyo ya ushindani mkali wa kukata kuwili.

Ni faraja kuona ulipoanzia hadi sasa kufikia kuwa miongoni wa Icons kwenye Bara la Africa.. Siku zote kumbuka, kila kazi ina mitihani na changamoto zake....jitahidi kuipokea kila inapokuja na kutafta njia sahihi ya kuishinda, maana tafsiri sahihi ya mtihani ni Kupanda daraja baada ya kufaulu,” Diamond alimvisha koja la maua Zuchu.

Alimalizia kwa kumhakikishi kuwa siku zote atasalia kumkubali na kumpenda licha ya masimango mengi kutoka kwa watu mbalimbali wanaobisha kuwa Zuchu hawezi tusua katika Sanaa ya muziki.

“Mwenyez Mungu akupe baraka na akulinde katika Maisha na safari yako hii ya kuchangia kuonesha Dunia kua WaAfrika tumebarikiwa kipaji kiasi gani… Kumbuka Simba siku zote anakupenda,” Diamond alimaliza kwa hakikisho kuntu.

Zuchu ambaye kwa sasa yupo Marekani kwa ziara ya muziki anasherehekea kufikisha miaka 29 na aliwataka mashabiki wake wote walioko Amerika kujitokeza kwa wingi Jumamosi hii katika jimbo la Seattle kwani atawaandalia bonge la shoo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

View Comments