In Summary

• Pia alisema kitu kingine kilichoweka mzigo mzito kwenye mabega yake ni kuachana na mpenzi wake mama wa mtoto wake.

Msanii Aslay apata mkataba na lebo ya Sony
Image: Instagram

Mwimbaji wa Bongofleva, Aslay kwa mara ya kwanza amefunguka kilichokwamisha safari yake ya muziki mwaka mmoja tu baada ya kusambaratika kwa kundi la Yamoto Band ambapo walikuwemo yeye, Mbosso, Enock Bella na Beka Flavour.

Kupitia filamu aliyoiachia kwa vipengele vitano kwa jina ‘Mimi Ni Bongo Fleva’ Aslay alipata kuzungumzia mengi yaliyotokea mpaka kupelekea yeye kupotea kabisa katika mwanga wa muziki wa Bongo Fleva.

Alisema kuwa aliingiwa na msongo wa mawazo baada ya kutaarifiwa kifo cha mamake aliyefariki usiku akiwa anatumbuiza Dar es Salaam lakini yeye akaja kutaarifiwa asubuhi.

Pia alisema kitu kingine kilichoweka mzigo mzito kwenye mabega yake ni kuachana na mpenzi wake mama wa mtoto wake – jambo ambalo lilimzamisha kwenye lindi la mawazo mpaka kufanya udhubutu wa kuingilia mambo ya ulevi na wanawake pia.

Katika kipindi hicho, wengi walikuwa wanalonga yao lakini yeye mwenyewe amefunguka kuwa alitafutwa na rekodi lebo tatu marufu nchini Tanzania ambazo zilitaka kumpa mkataba wa kufanya kazi nao lakini anasema kuwa alizikataa zote kwa sababu za kibinafsi tu.

“Kila mtu alikuwa anataka kufanya kazi na mimi, na kikubwa zaidi Lebo kubwa tatu zilinifuata ili kufanya nao kazi, siwezi kuzitaja ila kila moja ilikuja kwa njia yake jinsi inavyotaka kufanya kazi na mimi” amesema.

“Lebo ya kwanza ilikuja, walivyonielezea sikupendezewa na mikataba yao, jinsi wanavyotaka, kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda sana kujiamini, yaani mtu fulani wa kujitoa, kwa hiyo sipendi sana kubanwa kwenye kazi zangu, hivyo nilishindwa kusaini” alisema Aslay.

 

Aslay hivi karibuni alitambulishwa na lebo ya RockStar na Sony Music baada ya kuandikishwa mkataba wa kufanya kazi nao.

Katika Makala hayo ambayo ameyaeleza kwenye YouTube yake, Aslay alieleza kuwa ilimchukua muda mrefu sana kukubali mkataba huo kutokana na dhana iliyokuwa ikitambishwa na wasanii wenzake kuwa ukipewa mkataba na kampuni hizo basi huwezi fanikiwa kwani utafungiwa katika mambo mengi.

Aslay ameungana na Ommy Dimpoz, Abigail Chams na Young Lunya ambao wanafanya kazi na Lebo hizo upande wa Tanzania.

View Comments