In Summary

• Wataalam wanasema choo hicho kina uwezo wa kumpangusa mtu na pia kukausha baada ya kumaliza shughuli.

DJ Khaled afruahia Drake kumnunulia choo
Image: instagram

Msanii kutoka Marekani, DJ Khaled amemmiminia sifa kocho kocho msanii mwenzake kutoka Canada, Drake baada ya kumpa zawadi ya vyoo 4 vyenye haiba iliyotukuka.

 

Khaled kupitia Instagram yake, alipakia video akiwa katika choo hicho kimoja cha kuhamishwa na kumwaga sifa na shukurani zake kwa Drake kuwa alichompa kama zawadi ni moja ya vile vitu ambavyo alikuwa anavitamani katika orodha yake.

“Mimi na malkia wangu tumekuwa tukitaka hii kwa nyumba yetu!! 😱😱 asante ndugu yangu!! Nahhh hiki si choo cha kawaida 🚽 hii hiyo TOTO! Mfano sawa na wale wa ubalozini 🇨🇦 NAPENDA JINSI GANI DRAKE!! Upendo kaka!! Asante kwa zawadi 🎁 PS usisahau mambo mengine tuliyozungumza - kumbuka Chef Melissa na Nicole walikuwa mashahidi wakati U kusema ni mpango uliokamilika 👀🤫Nakupenda kaka! Wewe ndugu yangu milele!” DJ Khaled alisema.

Zawadi aliyopokea DJ Khaled ina bakuli la choo linalojumuisha mfumo wa kusafisha wa UV, udhibiti wa mbali, kufungua na kufunga kiotomatiki, utendaji wa bidet, na kiondoa harufu cha hewa kilichojengewa ndani. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, vyoo vya baadaye vya Drake vina thamani ya KSh 7.3m kila kimoja.

Alisema ataweka bakuli moja kwenye studio mahususi kwa ajili ya Drake ili aweze kufurahiya anapotembelea, lingine kwenye chumba chao cha kulala na chumba cha kulala wageni pia ili wageni wao wajue raha ni nini.

View Comments