In Summary

• Pongezi kwa wazazi wote mnaoendeleza uzazi kwa kuwa karibu na watoto wenu, mnafanya kazi kuntu - Namu alisema.

• Namu ni mama kwa watoto wawili ambao wameachana kwa miezi kadhaa tu.

Ivy Namu, mpenzi wa Willis Raburu akiwa na wanawe wawili
Image: Instagram

Mpenzi wa mtangazaji Willis Raburu, Ivy Namu amefunguka kuwa kwa wiki kadhaa tangu kumpokea mtoto wa pili, amekuwa akilemewa sana kusawazisha katia ya mambo tofauti kwenye maisha yake – haswa kutokana na jukumu gumu la kumlea mtoto mchanga.

Namu kupitia Instastory yake, ameandika ujumbe mrefu akieleza jinsi ulevi umemtwika jabali zito kichwani huku akishindwa hata kujizingatia mwenyewe na hata kutangamana na marafiki zake kwenye mitandao ya kijamii, kinyume na ilivyokuwa awali akiwa bado hajapata mtoto.

“Kwa wiki kadhaa zilizopita nimekuwa nikijihisi kulemewa kabisa kutokana na kuwa karibu na kwa makusudi yote na wanangu, na pia kupata muda wangu binafsi pia. Na pia kupakia vitu hapa ndio kumepata pigo kubwa zaidi, na kwa kweli sijielewi kabisa na hilo,” Namu alisema.

Alizidi kuelezea kwamba sasa imembidi kufuata mkondo huo wa kuendelea kuwa mchache mitandaoni kutokana na jukumu kubwa la kuwaangalia watoto wake wawili ambao wameachana kwa miezi kadhaa tu.

“Kwa hiyo ninaenda tu na mkondo huo wa kupakia mara chache, ninachokitaka sasa hivi ni kupata nafasi ya kupumua basi tosha. Lakini watoto wawili si wachache, kusema kweli ni kazi ngumu sana kuwalea watoto. Pongezi kwa wazazi wote mnaoendeleza uzazi kwa kuwa karibu na watoto wenu, mnafanya kazi kuntu.”

Wengi walionekana kutoelewa ujumbe huo wake kwa haraka na Namu hakuchelewa kujitetea kwa kusema kwamba akili yake imetapakaa kote kote kwa hiyo kuwataka wawe waelewa.

“Nahisi kama akili yangu iko kila mahali, niwie radhi kama sijagonga ndipo katika ujumbe wangu, nafikiria sana kwa sauti,” Namu alisema.

Miezi kadhaa iliyopita, Namu na Raburu walitangaza kupata mtoto wa pili wa kike takribani mwaka mmoja na miezi ya kuhesabika tangu kumkaribisha mtoto wa kwanza wa kiume waliyempa jina Mali.

View Comments