In Summary

• "Hongera binti yangu kwa kukamilisha mtihani wako kwa ujasiri, naamini kuwa ulifanya vyema. Natumai matokeo yatakuwa ya kupendeza," Terence aliandika.

Terence na Binti yake
Image: Screen Grab

Msanii Terence Creative amemtakia binti kifungua mimba wake, Luizer Mwangi kila la heri huku akisubuiri matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane.

Kwenye Instastory yake, Terence aliweka picha ya mke wake na Luizer na kumwandikia ujumbe na matumaini yake kwake.

"Hongera binti yangu kwa kukamilisha mtihani wako kwa ujasiri, naamini kuwa ulifanya vyema. Natumai matokeo yatakuwa ya kupendeza," Terence aliandika.

Hivi majuzi alipakia video akiwa kwenye hafla ya kuwaombea watahiniwa shuleni mwa binti yake.

Alimpa moyo bintiye na kumwambia kuwa ana uwezo wa kuwa mwanafunzi bora.

"Hamna shinikizo, nakutakia mema katika mtihani wako," Terence alisema

Luizer aliwaambia watu wamwombee na ana imani kuwa atafaulu kwenye mtihani wake wa kitaifa.

"Binti yangu, binti yangu, unawezana na hili na najua kuwa utafaulu, nakubariki na Mungu awe nawe. Nakutakia furaha unapoufanya mtihani huo," Terence aliandika.

Mke wake, Milly Chebby pia alimtakia binti huyo wa Terence kila la heri kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Mtahiniwa wetu ana ujasiri mno. Nakutakia kila la heri unapojitayarisha kuufanya mtihani wako Luizer Mwangi," Milly aliandika.

Terence ni miongoni mwa watu maarufu ambao watoto wao wameufanya mtihani wa kitaifa mwaka huu.

Miongoni mwao ni Bahati na Diana Marua ambapo mtoto wao wa kuasili, Morgan Bahati alikuwa mtahiniwa wa Gredi ya 6.

Kwenye Instagram, Bahati alisema kuwa ana matumaini Morgan atafaulu kwenye mtihani huo.

"Nikitazama jinsi tulivyotoka mbali, siwezi kuamini kuwa mwanangu ni mtahiniwa mtarajiwa wa mtihani wa kitaifa wa darasa la 6. Utukufu kwa Mungu unapojitayarisha kujiunga na Junior High," Bahati alisema.

View Comments