In Summary

β€’ Kwenye Instagram, Omondi na Cartoon wamekuwa wakipakia picha wakiwaiga wanamuziki hao kivyao ila sasa wameungana na kujifanya wapenzi.

Eric Omondi na Cartoon Comedian// Diamond na Zuchu

Mchekeshaji Eric Omondi na Cartoon Comedian wameungana kuwaiga wanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz na Zuchu ambao walifichua kuwa wapenzi hivi majuzi.

Kwenye Instagram, Omondi na Cartoon walipakia picha wakiwaiga wanamuziki hao kivyao ila sasa wameungana na kujifanya wapenzi hao.

Wachekeshaji hao walivaa na hata kuzungumza kama Diamond na Zuchu na kutumia wimbo wa Zuchu wa 'Kwikwikwikwi kuashiria wanayezungumzia.

"Mtu na Boss wakeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚," Omondi aliandika huku kwenye video aliyopakia akiiga mitindo ya kuvaa ya Diamond.

Hivi majuzi, Cartoon alikuwa amepakia video akimwiga Zuchu akieleza jinsi yeye na mpenzi wake Diamond walianza kuchumbiana.

"Najua mnaniuliza kuhusu ndoa yangu na Mondi. Tulipoanza, Mondi kaanza kunigusa, mwanzo nilikuwa naogopa lakini ikafika muda nikauzoea mkono wake maanake wajua yeye ndio Simba.Kaanza kunibusu kidogokidogo nikampenda kisha nikaanza kutoa nyimbo nzuri.Ana gemu kweli," 'Zuchu' alisema.

Cartoon alikuwa na muundo wa nywele kama wa Zuchu na hata kuvalia miwani kama yake.

Wachekeshaji hao wamekuwa na mitindo ya kuwaiga watu maarufu wengine huku Omondi pia akiwa na mitindo yake ya kuvaa ya kusisimuai kiwemo kuvalia kama mwanamke.

Cartoonn hata hivyo, kando na kuwaiga watu maarufu amekuwa akiiga tamaduni za Kenya kama mtindo wake wa kuchekesha watu.

Omondi vile vile amewaiga watu marufu kama vilerais Ruto, Zuchu, Diamond na hata mwanawe rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi.

Aliiga jinsi Muhoozi atakavyochanganyikiwa iwapo atajaribu kuteka jiji la Nairobi kama alivyosema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Ujumbe aliokuwa akijaribu kupitisha ni kuwa iwapo Muhoozi angejaribu kuvaamia Kenya angechanganyikiwa kwa mazingira yake mazuri marefu, wanawake na mihadarati na hata kuporwa mjini Nairobi.

View Comments