In Summary

• “Na wakikupenda kweli watakuheshimu na kuheshimu kile kinachokufanya ustarehe na upate utulivu,” alisema Bahati.

Bahati akiwa na mkewe Diana Marua.
Image: Instagram

Msanii bahati ameachia ushauri nasaha kwa wapenzi huku akiwahimiza kuheshimu chaguo la kila mmoja katika uhusian.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati aliwataka watu wanaopendana kutoshinda muda wote wakifuatilia kile ambacho wenzao wanafanya kwani kama unampenda mtu, unafaa kumpa uhuru wake afanye kitu ambacho kinamzidishia furaha.

“Upendo ni huria. Upendo haulazimishi. Ukimpenda Mtu mruhusu afanye kile Kinachomfurahisha,” Bahati alisema.

Alizidi kueleza kuwa unapompa mwenzako uhuru wa kufanya kile anachokipenda, basin aye kama anakupenda pia bila shaka atajibu kwa kukuheshimu na kile ambacho kinakupa faraja na utulivu wa moyo.

“Na wakikupenda kweli watakuheshimu na kuheshimu kile kinachokufanya ustarehe na upate utulivu,” alisema.

Ushauri huu wa Bahati unakuja wiki kadhaa baada ya watumizi wa mitandao ya kijamii kumsulubisha kwa kuoa Diana Marua ambaye alikuwa amechumbiana na wanaume wengi kabla ya kuoana naye.

Kusutwa huku kulikuja baada ya Wakenya kuibua video ya Marua ya mwaka 2020 akifunguka makubwa kuwa maisha yake ya awali yalikuwa si ya kusimuliwa kabisa. Alieleza kuwa kutokana na mazingira magumu ambayo alilelewa, alilazimika kuanza kutafuta pesa akiwa mdogo ili kukimu mahitaji ya wadogo zake.

Na hivyo ndivyo aliishia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa, baadhi wakiwa wale wenye wameoa. Alisema kila hitaji lake lilikuwa na mwanaume maalum wa kulishughulikia.

Kwa wakati mmoja, watumizi wa mitandao ya kijamii waliibua picha yake ya zamani wakimtuhumu kuwa aliwahi kuchumbiana na mbunge Jalang’oo lakini mbunge huyo alijitokeza wazi na kukanusha huku akisema ni urafiki tu wa kawaida.

Bahati na Diana Marua mpaka sasa wamebarikiwa na watoto watatu. Msanii huyo anazidi kutamba kwa kibao chake kipya cha Abebo alichomshirikisha mfalme wa Ohangla, Prince Indah.

View Comments