In Summary

• Jones alishauri kuwa kama safari ni ya chini ya saa moja, hakuna haja kutumia choo cha ndege na badala yake unafaa kujikaza hadi ndege itue.

Image: Hisani

Msanii wa rap Khaligraph Jones wikendi iliyopita alichukizwa na kitendo cha abiria aliokuwa ameabiri nao ndege kutumia choo ya ndege wakati safari yao ilikuwa ya dakika 40 tu.

Jones alisema kuwa tabia hiyo ilimkera kwani mtu anarudi kutoka uani na harufu yote kitu ambacho alisema mazingira katika ndege hiyo yaligeuka na kuwa na harufu ya kinyesi cha binadamu mtu mzima aliyekomaa.

Msanii huyo alichukua nafasi hiyo kuwashairo wasafiri kuwa haina haja mtu kuenda chooni ndani ya ndege wakati safari ni ya chini ya saa moja huku akiwashauri kujikaza mpaka washuke ndege na kuenda katika choo mbadala.

“Nashangaa sana na watu wanaenda kwa vyoo vya ndege kujisaidia wakati safari ni ya dakika 40. Shikilia hiyo kitu mpaka tutue uwanjani. Ndege imenuka kinyesi leo,” Jones aliandika kwenye instastory yake huku akimalizia na emoji ya kutapika.

Kauli hiyo ya Jones ilisambazwa pakubwa mitandaoni baadhi wakitaka kujua ni ndege gani hiyo aliabiri na abiria waliosababisha hali ya hewa ya ndege kubadilika walikuwa ni kina nani.

Wengine walitofautiana na ushauri wake wakisema kuwa dhima ya choo kwenye ndege ni kujisaidia hata kama unaruka kwa dakika 5 na haja ikubane mkiwa angani hakuna haja ubane wakati unajua kuna choo safarini.

View Comments