In Summary

• Madowo ni mwanahabari wa runinga ya kimataifa ya CNN na alikuwa nchini Qatar kufuatilia mechi ya nusu fainali.

Larry Madowo na Rio Ferdinand
Image: Twitter

Mwanahabari wa kituo cha kimataifa cha runinga CNN, Larry Madowo ni mu mweney furaha baada ya kukutana na aliyekuwa beki matata wa timu ya Manchester United, Rio Ferdinand katika moja ya viwanja vinavyotumiwa kuandaa mashindano ya kombe la dunia huko Qatar.

Madowo alifurahia wakati mzuri na mchezaji huyo wa zamani na hakusita kupasua mbarika kwa habari hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo alisema kukutana na mtu ambaye alikuwa anamtizama kwenye runinga ni kama kufanikisha ndoto yake.

Pia aliwashauri wanaume kuwa kama mpenzi wako wa kike hajui Rio Ferdinand ni nani basi wewe kama mwanaume jua huyo ni mdogo sana na hafai kuwa mpenzi wako.

“Nilikutana na Rio Ferdinand kabla ya mechi ya Ufaransa Morocco. Ikiwa hajui Rio ni nani, yeye ni mdogo sana kwako kaka!” Madowo alisema.

Wafuasi wake na ambao walikuwa mashabiki sugu wa kandanda na premia Uingereza EPL walimtaja Ferdinand kwa kumbukumbu mbalimbali huku wakimtaka Madowo kutuma salamu zake.

“Hii inanikumbusha wakati Manchester ilipokuwa Manchester United...uyu ni bazenga..Rio Ferdinand ni mtu mwenye bahati sana,” Mbaya Ken aliandika.

“Lwejendari wa Man U tunamfahamu sana, nisaidie kumuuliza anakumbuka Gareth Balamy na man city ni nani?” Collins Anderson aliuliza.

Wengine walichambua kauli yake na kusema kuwa ikiwa watapata wapenzi wasiomjua Ferdinand, huenda watawasamehe lakini katu hawawezi kusamehe iwapo hawatakuwa wanamjua Messi.

View Comments