In Summary
  • Mwanabiashara maarufu Anerlisa Mungai kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wasichana hao
Anerlisa Muigai
Image: Anerlisa Muigai/INSTAGRAM

Je kama mwanamke umewahi furahia kumchumbia mwanamume ambaye anafamilia yaani mke na watoto?

Ni mtindo ambao wasichana wachanga kutoka chuo kikuu wamejizoesha kwa kuwachumbia wanaumee ambayo tayari wwana familia.

Aidha wanaume wenyewe hawajalaza damu kwani wamekuwa wakikimbizana na wasichana hao, huku wakidai kwamba wana damu joto.

Mwanabiashara maarufu Anerlisa Mungai kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashauri wasichana hao.

"Wakati wa ukimya kwa wale wanawake wanaokuja kwenye uhusiano wakidhani watakuwa bora kuliko mke

Shida ni kwamba unaona wanaume wanapendeza kwenye mitandao ya kijamii, bila kujua kuwa mke ndiye aliyemuweka pamoja kwa hiyo ukipewa nafasi hiyo huwezi kuendelea na hilo."

Je unaweza tamani kuwa na mwanamke mwingine bali na mke wako, au kama wewe ni mke unaweza fanya aje ukimpata mwanamume wako na mwanamke mwingine, na bali sio wa umri wwako lakini ana umri wa chini.

Wengi wamejipata katika hali hiyo na kisha kuwaacha waume zao, kwani huwa wanahisi kusalitiwa.

View Comments