In Summary

• Watu walimjia juu kwa kumwita mtu anayehubiri maji lakini nyuma ya pazia akinywa pombe.

• Amekuwa akichukia wasanii wa kigeni kutamba Kenya ilhali yeye bado anatumia miziki yao kufanya mitikasi yake.

Eric Omondi akiiga Diuamond katika kudensi
Image: Instagram

Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi amejipata pabaya baada ya kupakia video aina ya reel kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anatumia wimbo wa msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz, Chitaki.

Bilas haka hili lilikuwa linatarajiwa kutoka kwa  baadhi ya wafuasi wake kutoka Kenya ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimsubiri kuteleza kidogo katika azma yake ya kuwahubiria Wakenya umuhimu wa kupenda na kukumbatia vilivyo vyao.

Omondi kwa muda mrefu amekuwa akikejeli vyombo vya habari nchini Kenya na Wakenya kwa kijumla katika kle alisema kuwa wameasi miziki ya humu nchini na kukumbatia miziki ya kutoka nje haswa Tanzania na Nigeria.

Alianzisha kampeni za kutaka miziki ya Kenya kupewa kipaumbele kwa asilimia 75 katika kile aliweka chini ya alama ya reli ya Play75%KE.

Mchekeshaji huyo mpaka alikwenda bungeni kupeleka mswada wa kutaka kupitishwa kuwa sheria kwa vyombo vyote vya habari nchini kupatia miziki ya Kenya kipaumbele kwa asilimia 75.

Lakini hatua yake ya kutumia muziki wa Diamond katika reel yake ilionekana kukinzana na kampeni hizo zake huku wengi wakimtaja kama mtu ambaye anahubiri maji lakini nyuma ya pazia akibugia divai.

Baada ya kupakia reel hiyo, Wakenya walimshambulia vikali na hata kumtaka kujionea aibu kwani haiwezekani yeye ndiye yuko mstari wa mbele kupinga miziki ya kigeni hali ya kuwa yeye  bado anaitumia katika sekeseke zake mitandaoni kuendeleza brand yake.

“Play 75% ke music na yeye mwenyewe anatumia ngoma ya Diamond kwa reels….

Kundi la watu wa kujifanya sana hawa,” aliandika d_town_kid.

"Huyu ndiye balozi mwanzilishi wa kucheza muziki wa 75% wa Kenya unaovuma 25% ya muziki wa TZ," aliandika Omarike.

“Huyu ndiye mfano wa wachungaji na wahubiri wa siku hizi, hadharani anawahubiria kuwa pombe ni mbaya lakini faraghani kwenye jokofu lake amejaza bia na pombe kali kali za kila aina,” mwingine aliandika.

 

View Comments