In Summary

• Grace, ambaye alikuwa akipenda nguo hizo alisema zilikuwa za joto na alikuwa amemnunulia jozi kadhaa.

Ekirapa na mumewe na mtoto wao AJ
Image: Instagram

Mwanahabari Grace Ekirapa amewachekesha mashabiki wake mitandaoni baada ya kupakia video akiwa amemvalisha mtoto wake AJ nguo kubwa zilizompwerepweta.

Ekirapa alitetea hatua yake kumvisha mtoto nguo kubwa kuliko umri wake kwa kusema kuwa alilazimika kufanya hivyo kwa kuwa mtoto huyo anakua kwa kasi ya 5G.

Alisema kuwa alifanya hivo kama kina mama wa Kiafrika wa zamani ambao walikuwa wananunulia watoto nguo na viatu vikubwa ili kua navyo pindi umri unavyokwenda ndio nguo hizo zinazidi kuwatoshea.

Ekirapa ambaye ni mpenzi wa mwigizaji Pascal Tokodi alisema amechoka kumnunulia nguo zinazomtoshea ambazo anaishia kuzivaa kwa wiki moja tu kisha kuziacha kwa kuwa ndogo za kumbana.

“Kwa vile AJ anakua mrefu kila siku nimeamua kuwa mama wa kiafrika kweli na kununua nguo kubwa zile atavaa hadi darasa la 1 alaaa🙄 nimemnunulia nguo saizi yake kisha anavaa wiki moja na anakua hivyo nimecheza kama mimi,” Ekirapa alisema.

Grace, ambaye alikuwa akipenda nguo hizo alisema zilikuwa za joto na alikuwa amemnunulia jozi kadhaa mtoto wake anayekua daima. Mtoto AJ alionekana kustarehe katika nguo za begi alizopewa na mama yake mpendwa akiwa amelala kitandani.

Mashabiki wake hakuweza kulinyamazia hilo kwani baadhi walikubaliana naye kuwa siku hizi watoto wanakua kwa kasi mno na ni vizuri kuwatangulia mbele ya ukuaji wao kwa kuwasitiri kwa nguo kubwa ambazo miili yao itazipata mbele ya safari.

“Ni miezi mingapi mbeleni umenunua, nipe ushauri mzuri ninakumbwa na tatizo sawia,” Judy Misati aliuliza.

“Wanaonekana wazuri kwake na ndio, watoto wachanga hukua nguo zao haraka sana.” Mwingine alisema.

View Comments