In Summary

• Uganda waliwakilishwa na Salvado huku Tanzania wakiwakilishwa na Joti na Jolmaster.

Omondi na Trick ywaongoza kenya kweney orodha ya wachekeshaji ya BBC
Image: Instagram

Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi na mwenzake MCA Tricky waipeperusha vyema bendera ya Kenya katika orodha ya shirika la habari la kimataifa la BBC la wachekeshaji bora wa mwaka 2022 katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Omondi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijitambulisha kama rais wa uchekeshaji Afrika nzima aliongoza orodha hiyo huku MCA Tricky akishikilia nafasi ya nne.

BBC News Africa walitoa orodha ya wachekeshaji watano bora katika ukanda wa Afrika mashariki ambapo Omondi aliibuka kidedea.

Nchini Tanzania walichukua nafasi ya pili na ya tano kwa wachekeshaji Joti Official na Jolmaster huku Uganda wakijinafasi katika nafasi ya tatu kupitia kwa mchekeshaji wao wa muda mrefu Patrick Sallvado.

Omondi ambaye katika mwaka wa 2022 amekuwa akifanya vitimbi na vichekesho vingi vya kila aina alifurahia orodha hiyo na kusema kuwa ni wakati sasa watu waamini anapojiita rais wa uchekeshaji Afrika kuwa anamaanisha kweli wala si utani.

Mchekeshaji huyo ambaye katika mwaka huo aliona ufuasi wake mitandaoni ukikua kwa kasi mno sasa anashikilia rekodi ya Mkenya wa kwanza kufikisha ufuasi wa watu milioni 4 kwenye Instagram.

Eric amekuwa akifanya maigizo kuhusu kila kitu ambacho kinatokea ikiwemo matamshi ya mwanawe Yoweri Museveni aliyesema angeuteka mji wa Nairobi, hadi kuiga kuapishwa kwa rais William Ruto.

Omondi na Tricky bila shaka ni zao la mchekeshaji mkongwe Churchill ambaye aliwatambulisha stejini na kuwapa umaarufu ambao nao hawajamuangusha bali wamezidi kuipeperusha vizuri bendera ya Kenya na jina la Churchill ambaye wengi wanamtaja kama muasisi wa uchekeshaji wa kidijitali Kenya.

View Comments