In Summary

• Ng'ang'a pia alisema mama huyo ndiye alikuwa mtu wa kwanza kununulia wanakwaya wa kanisa lake sare.

Ng'ang'a amzawadi gari muumini wa kanisa lake
Image: Screengrab//YouTube

Mchungaji mwenye utata, James Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelical jijini Nairobi amemzawadi mmoja wa waumini wake na rafiki wa muda mrfu kwa kumpa gari kwa kudumisha urafiki tangu miaka ya 90.

Katika video ambayo ilipakiwa mitandaoni na ukurasa wa YouTube wa kituo chake cha runinga, Sasa TV, mchungaji huyo qalikuwa anahubiri kabla ya kumuita mwanamke huyo kwa jina Mama Mbugua kujongea mbele na kumwambia kuwa alikuwa na nia ya kumpa zawadi nzuri ya kuanza mwaka 2023.

Ng’ang’a alifunguka kwamba mwaka wa 1990 alipoachiliwa huru kutoka gerezani, alipata kazi yake ya kwanza ya kuuza matunda na Mama Mbuguaalikuwa mteja wake wa kwanza kumsapoti kwa kununua matunda, kando pia na kuwa waumini katika kanisa moja walikokuwa wakiabudu wote.

“Angalia huyu mtu, huyu mama tulikuwa naye kanisa ile niliingia, nilimkuta huko. Nimemuuzia maembe na mkokoteni kwa duka lake. Bwana yake alinipenda sana, alikuwa ananiingiza kwa hoteli yao na kusema ‘mpatie mchungaji kile anataka’. Naye huyu mama alikuwa anatoka hapo kwa mkokoteni yangu na kujaza maembe kwa mfuko wake, si kwamba hakuwa na uwezo wa kuenda sokoni bali alikuwa anataka kusapoti biashara yangu,” Ng’ang’a alisimulia mbele ya umati wa kanisa lake.

Mchungaji huyo pia alisema mama huyo alikuwa mtu wa kwanza kununulia waimbaji wa kanisa lake la kwanza sare za kufanya kazi ya bwana. Alimtaka mmoja wa wafanyikazi wa kanisa hilo kuongozana na mwanamke huyo hadi nyumbani kwake na kuchagua gari moja la kumpendeza ili kuondoka nalo kwenda Mombasa kama lake.

“Nenda naye nyumbani achagua gari lenye anataka aondoke nalo,” Ng’ang’a aliamrisha  mmoja wa wafanyikazi wake.

View Comments