In Summary

• Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Kioko na Wambo waliandaa sherehe ya kufichua ujauzito kwa kushirikiana na hospitali ya Komarock.

Nicholas Kioko na mpenzi wake
Image: Nicholas kioko,// Instagram

Mwnablogu Nicholas Kioko na mpezi wake hatimaye wameweka wazi jinsia ya watoto wao mapaja watarajiwa.

Wapenzi hao miezi kadhaa iliyopita walifichua kuwa walikuwa wanatarajia watoto mapacha ila hawakutaja jinsia.

Katika video ambayo walichapisha jana mitandaoni mwao, Kioko na mpenzi wake Ashley Wambo walifichua kuwa wanatarajia watoto wa kiume mapacha.

Hafla hiyo ya utambulisho wa jinsia ya watoto wao, wanablogu mbalimbali walihudhuria kuwapa shavu na kongole kwa hatua hiyo yenye kheri katika maisha ya wapenzi.

Kioko alimshukuru Mungu kwa kumpa Baraka hizo huku akisema anajihisi mwenye fahari kushuhudia safari yake akivuka kutoka ujanani hadi kuwa mzazi mtarajiwa.

“Asante Bwana kwa kutimiza ndoto zetu. Sisi sote hatuwezi kungoja kuwashikilia wavulana wetu hivi karibuni,” Kioko aliandika Instagram.

Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Kioko na Wambo waliandaa sherehe ya kufichua ujauzito kwa kushirikiana na hospitali ya Komarock.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kioko alipakia picha maridadi pamoja na kionjo cha video ya jinsi walifichua ujauzito wao na kusema kuwa ni Baraka kuwa na furaha kuwa ni baba mtarajiwa tena wa mapacha.

“Mioyo yetu imejaa🙏 Miale miwili midogo ya jua kutoka kwa Mungu. Tunayo furaha kuwatangazia kuwa tunatarajia mapacha. Tutashiriki safari yetu na nyinyi ....Mungu ni Mwema,” Nicholas Kioko alisema.

Wanandoa hao ambao wanajulikana kwa video zao za kusisimua za YouTube walikuwa wametania habari hizo kwa muda na kusababisha mashabiki kudhani baada ya kutangaza kuwa walikuwa na habari kubwa za kushiriki.

 

View Comments