In Summary

• Eric Omondi alisema wasanii wa injili wana skendo nyingi za kuwachafua kuliko zile ambazo zinawaandama wasanii wa sekula.

Pozee aahidi kusema kilichomtoa kwenye injili
Image: Instagram

Msanii Willy Paul ameonekana kujibu tamko la Eric Omondi kuwa alitoroka kuimba miziki ya Injili na kuzamia ya kidunia.

Katika video ambayo Eric Omondi alifanya na kuipakia kwenye Instagram yake, aliuliza uwepo wa wasanii wa Injili ambao walikuwa wanatunga nyimbo nzuri za kumtukuza Mungu, ambazo mcheshi huyo alisema ndizo zilikuwa kama nembo ya kulitambulisha taifa la Kenya.

Alisema kuwa wote walizama kusikojulikana huku pia akiibua madai ya ukakasi kwamba baadhi yao wanajihusisha na vitendo vya kuvunja amri ya saba katika mtaa wa Umoja jijini Nairobi.

“Yuko wapi Bahati, yuko wapi Willy Paul…. Nakumbuka enzi za tuzo za Groove ambazo zilikuwa kubwa Zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, halafu kitu cha mwisho nilisikia ni kwamba baadhi wanafanya mapenzi katika mtaa wa Umoja, Willy Paul aliacha injili na sasa wako na skendo nyingi kuliko wasanii wa sekula…” Omondi alisema.

Aliwaambia kwamba kwa vile wamemuacha Mungu, hawatoweza kufanikiwa katika maisha yao kamwe.

Tamko hili lilijibiwa na Willy Paul ambaye alisema atatoa ufafanuzi wa kina kuhusu kilichomuondoa katika Sanaa ya injili huku akisisitiza kwamba uhusiano wake na Mungu bado haujabadilika kama ambavyo Omondi alikwa anasema.

“Nitawaambieni kilichonitoa katika Sanaa ya injili lakini pia uhusiano wangu na Mungu uko pale pale haujabadilika,” Willy Paul aliandika kwenye Instastory yake.

 

View Comments