In Summary

• “Wewe kwanza unatembea uchi, unapata wapi ujasiri wa kuja kutoa ushauri kwa watu wako katika huduma ya injili?" - Syokau.

SYOKAU AMCHARUKIA VIKALI OMONDI
Image: InstaGRAM

Mwanamuziki wa injili ambaye pia siku za hivi karibuni amekuwa akijiita nabii wa kike, Justina Syokau ameonesha kero lake kwa mchekeshaji Eric Omondi akiwatuhumu wasanii wa injili kuwa wamepotoka kimaadili na wanakumbwa na skendo nyingi kuliko hata wasanii wa injili.

“Eric ukitaka kutrend, fanya ucheshi na usicheze na wasanii wa injili. Kuna kitu inaitwa usijaribu kugusa wateule wa Mungu. Unapozungumzia injili, kwanza mwenyewe nenda uokoke, na ubadilishe mavazi yako kwa sababu unazungumzia kuhusu ushoga wakati mwenyewe unavaa vipodoshi vya kike,” Syokau alionesha kero lake.

“Wewe kwanza unatembea uchi, unapata wapi ujasiri wa kuja kutoa ushauri kwa watu wako katika huduma ya injili? Watu ambao wamepakwa mafuta na Mungu, una nguvu gani, umetoa nguvu wapi? Wewe si mfano kwa watoto wa kiume ambao tunao sasa hivi…” Syokau aliongeza kwa ghadhabu ya juu.

Kando na hilo, Syokau alifunguka kuwa mipango yake ya siku za usoni ni kuanzisha kanisa lake mwenyewe.

Syokau alisema kuwa kwa sasa anaendesha mahubiri yake ya uponyaji kwenye mtandao wa Facebook na tayari watu kadhaa wamekuwa wakimtumia shuhuda zao jinsi maombi yake yamewafungulia Baraka na kuwapanulia mipaka.

“Mwaka huu tumesema maono tunayaandika chini na tunayafuatilia. Nitafungua kanisa lakini si wakati huu, kwa sasa nahubiri Facebook kila siku, nitatoa maono,” Justina Syokau alisema.

Msanii huyo mwenye utata mwingi alisisitiza kwamba yeye ni msanii wa injili anayejiongeza kama nabii wa kuhubiti na kupuuzilia mbali madai ya baadhi ya watu kwamba miziki yake pamoja ya mienendo ya kucheza densi si ya Kimungu hata kidogo.

“Mimi ni msanii wa injili, na ninahubiri, nilikuwa ninahubiri sana lakini ikafika mahali nikaona kanisani kwetu wachungaji ni wengi sana, nikasema wacha mimi nikuwe msanii wa kuimba injili, ule ujumbe tunaopewa kanisani niutunge kuwa wimbo,” Syokau alisema.

Ikumbukwe wikendi iliyopita mwenzake Size 8 alitangaza kuanzisha kanisa lake baada ya kupewa kibali kama mchungaji miaka miwili iliyopita.

 

View Comments