In Summary

• Msamaha huu ni kufuatia video ya Eric Omondi ambayo imekuwa ikipiga misele mitandaoni akiwatumbua wasanii wa injili.

• Mkubwa alisema kuwa hata kama si kweli lakini kuna wale pengine walijikwaa na kuwaombea msamaha kwa Mungu.

Solomon Mkubwa aomba msamaha kwa niaba ya Wasanii wa injili
Image: Instagram

Msanii wa injili kutoka jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye makau yake humu nchini Solomon Mkubwa ameomba msamaha kwa niaba ya wasanii wote wa injili wa Kenya kufuatia matamshi ya mchekeshaji Erick Omondi.

Katika mahojiano na mwanablogu mmoja wa humu nchini, Mkubwa alisema kwamba hakuan aliye msafi mbele ya Mungu na kuwataka Wakenya wawasamehe wainjilisti wote ambao kwa njia moja au nyingine huenda walijikwaa na kuanguka katika safari ya kueneza injili ya Mungu.

“Mimi nafikiria ni kwa sababu matamshi ya Eric Omondi yalikuja kwa njia ya waimbaji Zaidi, lakini watu wote wapo ndani. Ni nyota zinakuwa zinapigwa na hapo ndio unajua kuna tatizo. Lakini pia naomba msamaha, mahali tulikosea, tunaweza kuwa tulikosea tunaomba msamaha, Mungu atusamehe.”

 “Lakini hilo halitafanya injili ianguke maana injili bado inaendelea, watu wanaponywa. Naomba tu kwa wale ambao huenda tulikosea, tunaeza kuwa tulifanya usherati, tumekiri Mungu atusamehe. Mungu atuoshe. Naomba msamaha kwa niaba ya waimbaji,” Mkubwa alisema.

Mwinjilisti huyo aliendelea kwa kunukuu kitabu cha Mariko mlango wa 7 kifungu cha 21 akisema kwamba binadamu wote tunaishi na mapungufu 12 ndani ya mioyo yetu, ikiwemo usherati, mawazo mabaya, kiburi, upumbavu na kadhalika.

Wiki moja iliyopita mchekeshaji Omondi alipakia video akiwazomea wasanii wa injili ambao aliwataja majina baadhi yao akisema kuwa wamepoteza upako wa Mungu na sasa ndio wanaongoza katika matendo mabaya na skendo za kuchafua injili kucha-kutwa.

Matamshi hayo kwa Zaidi ya wiki mzima yamepokelewa kwa njia tofauti na baadhi ya makundi, wengine wakimkashifu kuwa anatafuta kiki na Sanaa ya injili. Hata hivyo kunao wengine wakiwemo wainjilsti wenzake na wahubiri ambao wamekubaliana naye wakisema kuwa aliwatumbua wasanii hao wanaojificha ndani ya Biblia lakini matendo yao ni maovu kupitiliza.

View Comments