In Summary

• Ng'ang'a alisema akiwa anahubiri Mombasa ,alimuombea Mjerumani mmoja ambaye alikuwa mgonjwa.

• Mjerumani huyo aliondoka kwenda kwao na kurudi mwezi mmoja baadae akisema amepona na kumtaka amwambia angependa amshukuru kwa kumpa nini.

• Ng'ang'a alimwambia angependa kuhubiri kwenye runinga na Mjerumani huyo akaifadhili ndoto yake runingani KBC.

Mchungaji Ng'ang'a azungumzia maisha yake kabla ya kuokoka
Image: Screengrab//SasaTV

Mchungaji mwenye utata anayejiita nabii wa Mungu James Maina Ng’ang’a amefunguka kwa kina kuhusu maisha yake ya utotoni kabla aanze kuwa mgeni wa mara kwa mara wa gereza la Nakuru.

Ng’ang’a ambaye alizaliwa katika eneo la Subukia kaunti hiyo ya Nakuru alisimulia kuwa baba yake alifariki mapema miaka ya 60 na huo ukawa ndio mwanzo wa madhira yake.

Baadae alihamia Kinangop akaandikwa kazi ya kukamua ng’ombe kwa tajiri mmoja. Baada ya kwenda jandoni, waliotoka na kosa lake la kwanza ambalo hakulitaja likampa tikiti ya kwenda katika jela ya Nakuru kwa miezi 6 mwaka 1972.

Ng’ang’a aliwashangaza waumini wa kanisa lake alipofichua kwamba kati ya mwaka huo wa 1972 hadi 1992 alikuwa ni mgeni wa gereza kila mara, huku ndani ya miaka hiyo ishirini akiwa anasherehekea Krismas nje ya jela mara mbili tu!

“Maisha yangu yalibadilikia mwaka 1972 na kutoka hapo hadi 1992 nilikuwa ndani na nje ya jela mara kwa mara. Katika miaka hiyo yote, ni mara mbili tu nilisherehekea Krismas nje ya jela,” Ng’ang’a alisimulia.

Mchungaji huyo alisema baada ya kuhangaishana na sharia, mwaka 1989 alimkubali Yesu kama mwokozi na kuokoka, aliacha kubugia mtindi na kuvuta sigara na bangi. Pia huo ndio mwaka alikiri makossa yake baada ya muda mrefu kwenye rumande. Akapewa kifungo cha ziada cha miaka miwili na nusu na mwaka 1992 akawa mtu huru.

Nje ya Jela

Ng’ang’a baada ya kuachiwa huru baada ya takribani miaka 20, dunia ya nje ya jela aliiona tofauti kabisa. Alijikuta jijini Mombasa na kwa sababu hakuwa na kisomo cha kumwezesha kupata kazi nzuri, alijikuta anafanya kazi ya umachinga na uhamali, kuchuuza maji na kubebea watu mizigo.

“Kwa sababu sikuwa na elimu, nilianza kubebea watu mizigo kule Mwembe Tayari na mkokoteni. Kutoka hapo nikapata mtu akanipa shilingi 500 nikanunua maembe na ndizi sokoni Kongowea nikaanza kujiuzia mwenyewe,” Ng’ang’a alisema.

Mchungaji huyo alisema alifunga ndoa na mke wake mwaka mmoja baada ya kutoka jela, mwaka 1993 na mwaka mmoja baadae  akafungua duka lake eneo la Bombolulu, pia akapata baiskeli na pikipiki za kurahisisha usafiri wake.

Hapo ndipo alianza kutembea kanisani miaka ya 1995 na baada ya kuvurugana na mchungaji wa kanisa, alipewa barua ya kufukuzwa kanisani na akaendelea kuhangaika hivyo hadi aliporudi Nairobi na kuanza kuhubiri kwenye runinga ya KBC baada ya kufadhiliwa na Mjerumani mmoja alioyemuombea

View Comments