In Summary
  • Kisha Shakilla aliweka rekodi sawa kwa kufichua kwamba walikuwa wamejadiliana kuanzisha familia kabla ya wawili hao kuachana
Shakilla amtumbua Kibe akijaribu kumtongoza
Image: Instagram

Ndani ya wiki chache baada ya kutangaza uhusiano wao mtandaoni, Flaqo na Keranta walikuwa wakivuma kwenye televisheni.

Miaka mitatu imepita tangu wawili hao waanze kuchumbiana. Lakini hawakufichua uhusiano wao kwa mashabii au wanamitandao hadi wiki moja kabla ya Siku ya Wapendanao, ndipo walipofanya hivyo.

Flaqo na Keranta walipakia video yao wakipima ujauzito siku ya Alhamisi.

Kwa kweli wanatarajia mtoto pamoja kwa sababu kipimo kilikuwa chanya. Walishiriki habari hizo za furaha na wafuasi wao, ambao waliwasifu kwa kupokea zawadi hiyo.

Mwanasosholaiti Shakilla kwa upande mwingine, bado hajashawishika kuwa Flaqo na Keranta wanapata mtoto pamoja.

Alishiriki rekodi yake na Flaqo ambayo walikuwa wametengeneza hapo awali. Alifichua kwamba aliwahi kuchumbiana na Flaqo siku za nyuma, na kumwaya mtama.

Alimtumia ujumbe, akisema haamini kwamba Flaqo alikuwa akishiriki ndoto waliyoshiriki miaka michache kabla na mtu mwingine.

Kisha Shakilla aliweka rekodi sawa kwa kufichua kwamba walikuwa wamejadiliana kuanzisha familia kabla ya wawili hao kuachana.

"Siamini ndoto tuliyokuwa nayo miaka 3 iliyopita sasa unaishi na mtu mwingie, hongera,"Shakilla aliandika baada ya kupakia video aiwa na flaqo.

 

 

 

View Comments