In Summary

• Msanii huyo alikuwa anazungumzia wimbo wake mpya "Amenitendea Zaidi"

• Alisema kwamba watu walikuwa wanamuita tasa lakini sasa ni mama wa watoto 3, mmoja akiwa amefariki.

Kambua, msanii wa injili akumbuka kuitwa tasa, kupoteza mtoto
Image: Instagram

Msanii wa injili Kambua ameachia wimbo wake mpya wenye mada ‘Ametenda Zaidi’ wimbo ambao anasema unampa kumbukumu zenye ukakasi mno jinsi alivyoitwa tasa kwa muda mrefu n ahata baada ya kufanikiwa kupata mtoto, akafariki baada ya siu mbili.

Msanii huyo kupitia video ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, alielezea chimbuko la wimbo huo alioutaja kama moja ya nyimbo zake pendwa uliandikwa na rafiki yake katiak huduma ya injili kwa jina Paul Clement.

“Nina furaha kubwa kuwatambulieshi huu wimbo wangu mpya wenye mada ‘Ametenda Zaidi’. Huu wimbo unaigusa roho yangu sana kwa sababu ni ushuhuda wangu. Lakini wimbo huu haukuandikwa na mimi, uliandikwa na rafiki wangu wa karibu Paul Clement, msanii wa injili kutoka Tanzania,” Kambua alisema.

Kambua alisema wimbo huo ulizaliwa baada yake kushiriki mazungumzo ya kina na Clement akimuelezea jinsi amekuwa akifikiria matendo ya Mungu katika maisha yake na baada ya kupiga tathmini nyuma, aligundua kwamba Mungu si tu alimtendea yale aliyomuomba bali alizidisha hata Zaidi.

Alisema kuwa pia mwezi wa Februari ambao ulikamilika Jumanne ni mwezi wenye kumbukumbu za aina yake kwake kwani ndio mwezi alimzika mtoto wake kipenzi.

“Mwezi wa Febaruari ni mwezi wa kipekee kwangu kwa sababu mwaka 2021 nilipata mtoto wa kiume wa ajabu ambaye Mungu alinipa. Nilimpata tarehe 12 na akafariki tarehe 14. Na kwangu mwezi huu unajawa sana na wingu jeusi la uchungu, na kukosa Imani kabisa lakini Mungu ameniinua kutoka kwa sehemu ya kiza kinene,” Kambua alihadithia.

Alisema kwamba anapotupa darubini nyuma kwa machungu yote aliyoyapitia kutoka kuitwa mwanamke asiyeweza kubeba ujauzito hadi sasa, anashukuru tu Mungu kwa kumtendea Zaidi.

“Ninaangalia nyuma mbali Zaidi ya kuvunjika moyo na kukosa Imani, kule nilikoitwa mwanamke asiyeweza kuzaa mpaka sasa nikiwa mama wa watoto watatu wa kipekee, mmoja yuko mbinguni na wawili wako name. mimi ni mbarikiwa, Mungu amenitendea Zaidi,” Msanii huyo alisema.

 

View Comments