In Summary

• "Kusema kweli mheshimiwa kama hujawahi chumbiana na Mkisii yeyote tunaamini wewe ni bikira,” Nyamu alitaniwa.

Karen Nyamu ataniana na Wakisii Facebook.
Image: Facebook

Jiji la Nairobi, sawa tu na sehemu nyingi nchini watu waliamka na habari njema ya mvua kunyesha baada ya kiangazi cha muda mrefu.

Wakaazi wa Nairobi hawakuchelewa kuonesha furaha yao kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, na seneta maalum Karen Nyamu ni mmoja wa walioonesha furaha yao kukaribisha mvua ambazo zilikuwa zimepotea hadi kufanyiwa maombi ya kitaifa yaliyoongozwa na rais Ruto mwezi mmoaj uliopita.

Katika kuonesha furaha yake, Nyamu aliwatania watu wa jamii ya Abagusii akisema kwamba alishangazwa kuona Mkisii akiwa na vumbi asubuhi jijini licha ya mvua kunyesha usiku kucha.

“Na hii mvua yote nimepatana na mkisii viatu viko na vumbi jijini 😂 Asante kwa mvua,” Nyamu alitania akimalizia kwa emoji za kucheka.

Hata hivyo, watu kutoka jamii ya Abagusii walifurika kwenye chapisho hilo na kumshambulia kwa utani mwingi, baadhi walimtaka kujaribu kuchumbiana na Mkisii mmoja ili kuwapa heshima.

Walimwambia kwamba akipata Mkisii mmoja wa kumchumbia, atamtoroka Samidoh kwani watu wa jamii hiyo wanajitapa kuwa ndiko chimbuko na kitovu cha mahaba na mapenzi yasiyojua kufa.

“Wewe unahitaji Mkisii akudhughulikie mpaka uhepe yule polisi, Wakisii huwa hatubembelezi watu ikifika ni ‘mambo hayo’. Kama ni shamba uliza Mkisii yeyote akwambie. Kusema kweli mheshimiwa kama hujawahi chumbiana na Mkisii yeyote tunaamini wewe ni bikira,” Sammy Ondimu Ngare, afisa wa polisi maarufu alimtania.

“Wewe ni kama hukupata Mkisii mahali akufanyie kile kitu, huwa hatuongelelewi sana na nyinyi,” Joshua Tree aliandika.

Mwingine alimtania kwamba hafai kufurahia sana juu ya kuona mvua kwani jambo hilo ni la kawaida mno katika eneo pana la Gusii.

View Comments