In Summary

• Mrembo huyo alisemwa kuwa mbadala wa Kajala Masanja katika maisha ya Harmonize baada ya kumpakia msanii huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Sishkiki amtaja aliyemnunulia Range Rover.
Image: Instagram

Mjasiriamali wa kuuza nguo Sishkiki Sikamatiki kutoka nchini Tanzania, mrembo ambaye wiki mbili zilizopita alisemekana kuwa mpenzi mpya wa msanii Harmonize hatimaye amezungumza.

Siku moja iliyopita, mwanadada huyo kwa mara nyingine tena aligonga vichwa vya habari za wambea baada ya gari jipya aina ya Range Rover kuonekana nje ya duka lake la nguo likiwa na jina lake kwenye sehemu ya namba za usajili.

Wengi waling’aka kwamba gari hilo li zawadi ambayo amekabidhiwa kutoka kwa msanii Harmonize, jambo ambalo hata hivyo alisita kulizungumzia huku akikataa katakata kuliweka wazi jina au maelezo ya aliyempa.

Hata hivyo, alikiri kwamba gari hilo ni zawadi aliyokabidhiwa na “mtu anayemdhamini sana” na kusisitiza kwamba hakuna kinachoendelea na Harmonize Zaidi ya urafiki tu.

“Harmonize ni mshikaji wangu, mwanangu kabisa. Tunajuana muda mrefu, ni mtu mzuri sana. Sitaki kuchokonolewa na lile Range Rover nilipewa na mtu anayenidhamini sana. Ila hapo kwa ni nani, sina maoni,” Sishkiki alisema.

Mrembo huyo alisemwa kuwa mbadala wa Kajala Masanja katika maisha ya Harmonize baada ya kumpakia msanii huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia kheri njema ya siku yake ya kuzaliwa wiki mbili zilizopita.

Sishkiki alimwandikia Harmonize ujumbe mzuri na kumalizia kwamba anatumai msanii huyo hayuko singo tena kwani yeye yuko.

Hata hivyo, Harmonize naye katika chapisho hilo aliwafanya wengi kukodoa Zaidi macho baada ya kusema kwamba mrembo huyo ni hatari na kumkaribisha katika maisha yake.

Ubadilishanaji wa jumbe hizo uliwafanya wengi kuwa na uhakika usiomithilika kuwa ni wapenzi, mpaka juzi kati za ndani zikaibuka kwamba mfuko wa Harmonize umehusika katika gari hilo lenye hadhi ya nyota tano.

View Comments