In Summary

• Mwanawe Davido, Ifeanyi alifariki mwezi Novemba mwaka jana, siku chache kuelekea kuanza kwa mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar.

• Tangu kipindi hicho, Davido hajakuwa akionekana sana wala kushiriki mahojiano yoyote.

Madowo akutana na Davido kwa mahojiano ya kipekee.
Image: Facebook

Mwanahabari wa kimataifa kutoka Kenya, Larry Madowo amebahatika kuwa mtu wa kwanza kuketi na msanii kutoka Nigeria Davido na kuwa na mazungumzo ya kina tangu msanii huyo aipompoteza mwanawe wa pekee mwezi Novemba mwaka jana.

Madowo ambaye amekuwa katika mataifa ya Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kwa muda akifanya mwendelezo wa habari za runinga ya CNN alidokeza kufanyika kwa kikao hicho na Davido.

Madowo alisema kwamba walikuwa na mahojiano yenye ufanisi mkubwa ambapo Davido alifunguka mambo mengi ya ndani kuhusu hali nzima ya kifo cha mwanawe na maisha baada ya msiba huo.

Mahojiano hayo yatapeperushwa kwenye runinga ya CNN hivi karibuni, Madowo aliwatamanisha mashabiki wake.

“Nilikaa na Davido kwa mazungumzo marefu na ya uaminifu - mahojiano yake ya kwanza tangu kupoteza mtoto wake. Yapate hivi karibuni kwenye Sauti za Kiafrika za CNN,” Larry Madowo alisema.

Davido ambaye amevunja kimya chake siku chache zilizopita kwa kutangaza albamu yake, amekuwa mwenye uchache mwingi mitandaoni tangu Novemba mwaka jana alipopigwa na msiba wa kifo cha mrithi wake, Ifeanyi.

Msanii huyo amekuwa akipitia wakati mgumu sana, kutokana na matukio yake mitandaoni, ambapo kwa kipindi kimoja alifuta picha zote Instagram na kuacha tatu tu, akiwa na mke wake Chioma, akitumbuiza kwenye jukwaa la kufunga mashindano ya kombe la dunia na ya mwisho ikiwa ya huyo marehemu mwanawe ambayo alikuwa amepakia kumtakia kheri njema ya siku ya kuzaliwa, siku chache kuelekea kifo chake cha ghafla.

View Comments