In Summary

• Wikendi iliyopita, Edday na Samidoh walikuwa wenye furaha na bashasha wakishuhudiwa binti wao akiongeza mwaka mmoja.

• Karen kwa upande wake alipakia picha ya Samidoh akiwa na yeye na binti yake pia siku ya kuzaliwa.

Nyamu asema Samidoh huwa anamuomba kofia yake.
Image: Insatgram

Seneta Karen Nyamu ameendeleza mashambulizi mazito dhidi ya mke mwenza, Edday Nderitu baada ya Samidoh kuonekana kwenye tukio la kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake na Edday.

Samidoh na Nderitu walivujisha rundo la picha kutoka kwa tukio hilo la mwanao wikendi iliyopita, ambapo kando na kuonekana pamoja, wachumba hao wawili pia walijitupa kwenye ukumbu na kusakata densi kwa wimbo wake mpya, Bado nakupenda – aliomshirikisha msanii wa Ohangla, Prince Indah.

Hata hivyo, tukio hilo halikupokelewa vizuri na Karen Nyamu ambaye haiishi vituko.

Nyamu alipakia picha akiwa chini ya mti akijivinjari lakini mashabiki wake waliamua kumuonjesha makali kuwa ako na upweke kwa sababu Samidoh yuko kwa mke wa kwanza.

“Wee Samidoh anakaa poa bado tuko kwa siku ya kuzaliwa na mtoto wa Edday, Nimo,” shabiki mmoja alimchokoza Nyamu.

Lakini kwa haraka Nyamu alizima chokoza hizo akisema kwamba kofia ambayo Samidoh alikuwa amevaa katika hafla hiyo ya mtoto wa mke mwenza ilikuwa yake.

Hio ilikuwa jana kamum anakaa poa sana na kofia yangu,” Karen alisema akimtupa Samidoh chini ya basi.

Ni muhimu kutambua kwamba siku zilizopita, Edday alidai kuwa yeye ni single na alizua uvumi kwamba hawataonana tena na baba mtoto Samidoh. Lakini inageuka kuwa ilikuwa uamuzi wa haraka ambao alifanya alipopata hisia.

Nyamu na Edday walihusika katika ugomvi katika klabu ya usiku ya Dubai mnamo Desemba 16, 2022, ambapo mwanamume wao alikuwa akitumbuiza, na kulazimisha walinzi kumfukuza seneta huyo aliyeteuliwa kutoka kwa taasisi hiyo. Tangu wakati huo, Nyamu aliahidi kuachana na biashara zao.

Lakini haikupita muda mrefu tena kabla ya kumparamia Samidoh, hatua iliyoonekana kukwamisha uhusiano wa msanii huyo na mke wa kwanza Edday.

Hata hivyo, Karen alimsifia Samidoh kama baba mzuri na kusema kuwa fadhila pekee wanafaa kumlipa kwa uzuri wake ni kumzalia watoto wengi.

View Comments