In Summary

• Chumba cha AJ pia kina sakafu ya zulia ya kijivu ambayo mamake alisema ilikuwa ya kuongeza joto.

• Pia waliongeza fanicha yenye droo zinazoweza kufungwa ambazo alisema ni mahali ambapo wanahifadhi vifaa vya kuchezea vya AJ.

Ekirapa na mumewe Tokodi wamzawadi mtoto wao wa miezi 11 na runinga
Image: Instagram

Wanandoa Pascal Tokodi na Grace Ekirapa wamepandisha viwango vya hadhi ya aina yake kwenye chumba cha binti yao AJ.

Mwigizaji huyo na mkewe mwanahabari walikuwa wanasherehekea miezi 11 ya kuzaliwa kwa mwanao na walifanya mabadiliko makubwa katika chumba chake.

Wawili hao walipakia video kwenye YouTube yao wakionesha jinsi wamerekebisha na kusasisha chumba cha mwanao ikiwemo kupakwa rangi upya na kumuongezea runinga ya kujivinjari kwa vipindi avipendavyo vya watoto.

Chumba hicho kina ukuta wenye picha za wanyama na Ekirapa alieleza kuwa hakutaka kumlazimisha binti yake rangi kwa vile watu wengi wangepaka rangi ya waridi ikiwa wangekuwa na binti.

Runinga bapa iliyowekwa ukutani na Grace alieleza kuwa atakuwa akiitumia kucheza nyimbo za mbelezi au nyimbo za kuabudu za ala ili kumsaidia AJ kupata usingizi.

Chumba cha AJ pia kina sakafu ya zulia ya kijivu ambayo mamake alisema ilikuwa ya kuongeza joto ndani ikilinganishwa na sakafu ya maroon ya awali ambayo haikuwa na vigae.

Pia waliongeza fanicha yenye droo zinazoweza kufungwa ambazo alisema ni mahali ambapo wanahifadhi vifaa vya kuchezea vya AJ na Grace aliongeza kuwa ataibadilisha kuwa rafu ya vitabu wakati binti yake atakuwa na umri wa kutosha kuelewa kazi za vitabu.

Katika kusherehekea miezi kumi ya kuzaliwa mwezi jana, wanandoa hao walimnunulia binti yao bidhaa ghali kama midoli ya kuchezea ya gari, baiskeli na vitu vingine vyenye thamani kubwa.

View Comments