In Summary

•Zari pia aliwapa wanaume vidokezo kuhusu jinsi ya kuwatendea wapenzi wao na jinsi ya kujua ikiwa wanawapenda.

•Zari aliwataka watu walio na wapenzi wa kweli kuwatunza huku akibainisha kwamba sio wengi wakweli wamebaki duniani.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasosholaiti maarufu wa Uganda, Zari Hassan alitumia sehemu ya wakati wake wa  usiku kuwashauri wanawake kuhusu masuala ya uhusiano.

Mama wa watoto watano pia aliwapa wanaume vidokezo kuhusu jinsi ya kuwatendea wapenzi wao na jinsi ya kujua ikiwa wanawapenda.

Kulingana na Zari, ikiwa mwanamke hamuudhi mwanamume aliye naye karibu kila siku, basi kuna uwezekano ana mpenzi mwingine.

"Ikiwa  mpenzi wako (mwanamke) hatakuharibia siku yako karibu kila siku, bila shaka anamfanyia hivyo mpenzi wake mkuu (mwanaume). Ikiwa tunachumbiana, huwezi kamwe kuwa na furaha 24/7. Nikiacha, hesabu hiyo kama bendera nyekundu," Zari Hassan alisema kwenye mtandao wa Instagram.

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo  Diamond Platnumz  aliwashauri wanaume kuwatunza wanawake wanaowapenda kwa dhati, huku akibainisha kwamba wengi wao wanachumbiana kwa ajili pesa.

Kwa upande mwingine, aliwapa wanawake ushauri wenye utata kuwa wanapaswa kusaliti penzi lao wanapopata fursa ya kufanya hivyo kwa ajili ya pesa. Akitetea kauli yake, alisema wanaume wana'cheat kwa sababu za kipuzi.

"Mtoto wa kike, ukipata nafasi ya ku'cheat kwa sababu ya pesa basi fanya hivyo. Hawa wanaume wana'cheat kwa mambo ya kijinga kama mapaja ya rangi ya kahawia, pete za ulimi na makalio makubwa. Saliti penzi kwa nyumba, Saliti penzi kwa kipande cha ardhi, saliti kwa gari la ndoto yako, ndivyo lilivyo," alisema.

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka  42 hata hivyo alijitenga na mambo aliyowashauri wanawake kuhusu na kusisitiza kuwa yeye huchumbiana kwa ajili ya mapenzi  na hayuko tayari kuwacheza na wanaume tofauti.

"Napenda mapenzi ya kale. Nataka kuwa na mtu wangu na kufanya kila kitu pamoja naye. Mambo madogo kama, kuendesha gari kwa njia ya kuchukua ice cream ya Mc Fluryy. Ni mambo madogo kwangu," Zari alisema.

Zari aliwataka watu walio na wapenzi wa kweli kuwatunza huku akibainisha kwamba sio wengi wakweli wamebaki duniani.

Kwa sasa, mama huyo wa watoto watano yupo kwenye mahusiano mazito na mwanaume Mganda mwenye umri wa miaka 31, Shakib Cham Lutaaya. Mahusiano ya wawili hao ya miezi kadhaa hata hivyo yamekabiliwa na ukusoaji mkubwa kutokana na tofauti kubwa kati ya umri wao.

View Comments