In Summary

• “Mara nyingi tu katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikiswali kuomba mume. Nahisi pesa ni muhimu sana" - Hamisa.

• Hata hivyo, Mobetto alisema hakuna tatizo kama mwanamume huyo atakuwa na pesa kidogo kumliko, lakini bora awe na pesa na mtu wa kujituma.

Hamisa Mobetto akizungumza kuhusu kutamani ndoa.
Image: Screengrab// YouTube

Mwanamitindo na mjasiriamali Hamisa Mobetto ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa msanii Diamond Platnumz amedokeza kwamba katika siku za hivi karibuni ombi kuu ambalo amekuwa akiliweka kwa Mungu ni kupata mume na ndoa.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba siku za nyuma hakuwa anaona umuhimu wa mume na ndoa lakini kadri siku na umri vinavyozidi kumpa kisogo, ameona kuna umuhimu mkubwa wa ndoa na amekuwa akiweka ombi hilo kwa Mungu.

“Kitambo nilikuwa naona kwamba sina Imani katika ndoa, kwa kipindi kile kweli nilikuwa sijawahi kuona mfano wangu kuwa nafaa kuwa na ndoa yangu kama baba Fulani na mke wake. Lakini sasa ndio naona umuhimu wa ndoa, ikizingatiwa kwamba sasa nina watoto na ninajua kwamba umuhimu wa mume utakuwa huu na ule, sasa naona mifano, naona vitu kwenye mitandao hadi nahisi tu kuolewa,” Hamisa Mobetto alisema.

Kinachomfurahisha katika mitandao ya kijamii ikiwemo Tiktok ambayo alisema ndio anaona mambo mengi ni jinsi watu wanachumbiana, akisema anapenda sana jinsi watu wanashtukiziana kwenye suala zima la kuchumbiana.

Lakini katika kupata huyo mume, Mobetto alisema kwamba anaomba kupata mume mwenye mihela.

“Mara nyingi tu katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikiswali kuomba mume. Nahisi pesa ni muhimu sana. Kama ninatia bidii sana kupata pesa ili kujukumikia watoto wangu na kila kitu, mume wangu naye lazima pia awe na pesa, nahisi ni vizuri ikiwa hivyo,” Mobetto alisema.

Hamisa Mobetto alisisitiza kwamba katu hawezi kumpenda mwanamume asiye na hela akisema kuwa kutoka zamani ni karia kwamba wanaume waliumbwa kutafuta na kujali familia zao.

“Sihisi kama mwanamume bila pesa ni vizuri, nahisi kwamba wanaume wameumbwa wajali familia. Mimi kumkubali mwanamume asiye na pesa hapana kwa kweli, mtanisamehe.”

Hata hivyo, alisema kwamba hana tatizo kumpenda mwanamume ambaye yeye anamzidi hela, bora tu awe ni mtu wa kujituma.

“Nikimzidi hela hakuna tatizo, nina uhakika akiwa na mimi hela zitaongezeka. Hata hivyo sijawahi chumbiana na mwanamume bila hela. Kwa sababu Fulani mimi pesa hunifanya kuwa nac furaha sana,” Mama mtu alitema ukweli wake.

 

View Comments