In Summary

• “Hakuna kitu cha kusema kwa sababu, unajua ni lazima watu wawe wanaongea, na mke wangu Sarah ako poa." Simon alisema.

• Pia mke wake alidhibitisha hilo akisema kuwa fikira na mawazo yake yalikuwa mbali wala hakuwaona Betty wakizungumza na mumewe.

Simon Kabu avunja kimya kuhusu picha yake wakicheka na Kyallo na mke wake akiwa anawanunia.
Image: Facebook

Mjasiriamali Simon Kabu amevunja kimya baada ya picha yake wakizungumza kwa furaha na mwanahabari Bety Kyallo huku mke wake Sarah Kabu kwa mbali akiwaangalia kwa chukizo kubwa usoni mwake kusambaa.

Picha hiyo ilinaswa katika tukio kubwa la mwanamuziki Akothee ambaye alikuwa anafunga harusi ya kifahari na mpenzi wake mzungu, Mr Omosh siku ya Jumatatu.

Simon wanaonekana wakicheka kwa furaha kubwa na Betty Kyallo huku mke wake akiwa ameketi kwenye meza ya nyuma pembezo ni akiwafuatilia kwa jicho la udukuzi, huku mfadhaiko mkubwa ukiwa umejichora usoni mwake kwa rangi ya kung’aa.

Hata hivyo, Simon amevunja kimya kuhusu picha hiyo iliyozua nadharia tofuati mitandaoni, baadhi wakisema kuwa mke wake hakuwa anafurahia mazungumzo na mumewe na Betty, lakini Simon amefutilia mbali mashaka hayo.

“Hakuna kitu cha kusema kwa sababu, unajua ni lazima watu wawe wanaongea, na mke wangu Sarah ako poa. Sasa atakasirika kwa nini. Unajua picha inaweza chukuliwa wakati ule mtu ameangalia hivi bila kuwa na ishu yoyote,” Simon alisema.

Mfanyibiashara huyo wa Bonfire Adventures alisema kuwa Betty Kyallo ni rafiki wake wa karibu sana na walikuwa wanazungumza mambo mengi tu kupelekea kuzaliwa kwa tabasamu lile ambalo lilionekana kuupasua moyo wa Sarah.

“Betty unajua ni rafiki wetu kwa muda mrefu. Jana nilizungumza na watu Zaidi ya elfu moja, si eti kuna kitu spesheli tuliuwa tunazungumza. Maneno ni mengi ya kuzungumza. Sisi ni marafiki wa kifamilia kwa muda mrefu na si kitu ambacho kinaweza wapa watu wasiwasi. Sarah yuko poa hana ishu,” Simon alidhibitisha.

Sarah kwa upande wake alisisitiza maneno ya mume wake akisema kuwa hakuwa na ubaya na Betty Kyallo kwa kutabasamiana na mumewe, huku pia akisema kuwa mawazo na fikira zake zilikuwa mbali na pale.

“Sikujua hata akili yangu ilikuwa mbali. Sasa unajua wakati mwingine unakuwa uko na fikira zako, hata sikujua wako hapo. Wakati mwingine akili inaenda mbali. Sikusikia vibaya baada ya hiyo picha, ni watu tuko kwenye biashara moja kwa hiyo hakuna kubwa baya. Betty ni rafiki yangu sana, yeye ni mteja wangu na kwa hiyo hatuna shida,” Sarah alisema.

View Comments