In Summary

• Baada ya KOT kudai kwamba albamu yake haikupata mapokezi mazuri, JuaCali alifutilia mbali madai hayi akisema mapokezi ni mazuri na ngoma zake zinatrend TikTok.

• Mwanamuziki huyo mkongwe anawataka mashabiki kuendelea kuunga mkono muziki wake na kupuuza masimulizi yoyote mabaya yanayosukuma mtandaoni.

uaCali afutilia mbali madai kwamba albamu yake ya Utu Uzima ilifeli.
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Kenya, Jua Cali, hachukulii kirahisi kelele za hivi majuzi za mtandaoni dhidi ya albamu yake mpya, Utu Uzima.

Msanii huyo aliamua kuvunja kimya baada ya sehemu ya watumizi wa Twittwr kudai kwamba albamu hiyo ambayo ilitoka siku chache zilizopita haijafanya vizuri na wala haikupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki wake.

Hata hivyo, Jua Cali ametumia mitandao ya kijamii kusafisha hali ya hewa na kuwahakikishia mashabiki wake kuwa muziki wake unafanya vyema kwenye majukwaa yote ya muziki.

Jua Cali alitolea mfano wa baadhi ya ngoma zake na kusema kuwa zilikuwa zinafnaya vizuri sana sit u kwenye majukwaa ya kupakuwa mizki bali pia kwenye mitandao ya kijamii kama vile TikTok.

“Mashabiki wangu! Msidanganywe na hawa wenye chuki wanaojaribu kusukuma simulizi fulani ya tasnia ya muziki imebadilika kwa sasa wimbo wangu wa kwanza ‘WAJAKOYA’ unafanya vizuri (Trending) kwenye TikTok na TikTok sasa hivi ndio kusema, YouTube ni sehemu tu ya mfumo wa ikolojia. Mashabiki wanasikiliza albamu kupitia nambari za majukwaa tofauti za UTU UZIMA Spotify, iTunes, Audio Mack, n.k hadi sasa ziko sawa,” alisema Jua Cali.

Msanii huyo alifutilia mbali dhana kwamba hakutoa miziki mizuri kwenye albamu hiyo, akifichua kwamba alichukua takribani miaka mitatu kuiandaa na kuwataka mashabiki kusikiliza muziki na kuupenda tu bila kushawishiwa na watu wa nje.

"Nilichukua miaka mitatu nzuri kurekodi albamu hii. Unapaswa kupenda muziki peke yako bila ushawishi wa nje. Baadhi ya watu tayari wanaiona kuwa ya kawaida, kwa hivyo ikiwa una wakati, sikiliza ‘Utu Uzima’ inayopatikana kwenye majukwaa yote ya utiririshaji. Asante, Wagenge,” alisema Jua Cali.

Mwanamuziki huyo mkongwe anawataka mashabiki kuendelea kuunga mkono muziki wake na kupuuza masimulizi yoyote mabaya yanayosukuma mtandaoni.

View Comments