In Summary

• Sarah miezi 5 iliyopita alidokeza kwamba mnamo Januari mwaka jana, aliharibikiwa na ujauzito wa vijusi mapacha.

Sarah amuuliza Simon Kabu mbona hawajashika mimba.
Image: Instagram

Baada ya mchekeshaji Jaymo Ule Msee na mke wake Catey Fortune kutangaza kupata mtoto nambari mbili chini ya mwaka mmoja, mjasiriamali Sarah Kabu amemsakama kooni mumewe Simon Kabu kutaka kujua ni kwa nini wao hawajapata mtoto hata mmoja katika kipindi hicho.

Sarah aliyaandika haya wakati anamhongera Jaymo Ule Msee na mpenzi wake na wakati huo huo kutupa swali kwa mumewe kuhusu ni kwanini wao hawajapata mtoto.

“Hongera Jaymo na Fortune, yaani Simon Kabu hata hatujashika wa kwanza,” Sarah aliandika.

Sarah Kabu

Miezi mitano iliyopita, Mkurugenzi huyo wa kampuni ya usafiri Bonfire Adventure alifichua kwamba aliharibikiwa na ujauzito.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Sarah alisema kwamba ingawa ni ngumu kutangaza hayo kwa mashabiki wake lakini imemlazimu kufanya hivyo ili kuliondoa dukuduku lililokuwa moyoni mwake.

Sarah alisema kuwa Januari mwaka jana, ujauzito wake wa mapacha ukiharibika.

"Hii ni ngumu kuandika lakini wakati mwingine nilipoteza mapacha wangu mnamo Januari 😢 ninamwamini Mungu kwa muujiza mwingine siku moja. Marafiki zangu maombi yanafanya kazi 💪 @kabusimon Asante kwa kusimama nami katika nyakati ngumu," Aliandika Sarah

Jaymo aliwashangaza wengi kutangaza kupata mtoto wa pili licha ya kuficha suala hilo kwa muda, ikizingatiwa kwamba miezi 13 tu iliyopita ndio walitangaza kupata mtoto wa kwanza wa kiume na mke wake Catey Fortune.

Safari hii familia hiyo ilibarikiwa na mtoto wa kike na kuingia kwenye orodha ya watu waliozaa watoto kwa kufuatana kwa ukaribi baada ya Willis Raburu na mkewe Ivy Namu.

View Comments