In Summary

• Msanii huyo alisema kuwa bado yungali mchanga sana kutoa hatma kwamba hawezi pata mapenzi ya kweli baina ya utajiri wake.

Harmonize akanusha kuwa mseja daima.
Image: Instagram

Harmonize, msanii kutoka Konde Gang anayetamba kwa kibao ‘single again’ amefunguka ukweli wa wimbo huo na kufutilia mbali uwezekano wa kusalia bila mpenzi katika maisha yake yote.

Katika video moja ambayo imeenezwa mitandaoni, Harmonize anasema kwamba hawezi kuishi maisha ya useja milele kwani yeye bado ni kijana mbichi, tajiri na angalau ana utanashati kwa kiasi kikubwa cha kukubalika na mabinti wengi.

“Mnadhani eti nitakuwa singo daima, hapana. Siwezi kuwa singo maisha yangu yote kaka zangu. Mimi ni mchanga, ni tajiri na pia ninavutia kwa utanashati kiasi, kwa hiyo mbona niwe singo daima? Siwezi!” Harmonize alisisitiza akicheka kwa utani.

Msanii Harmonize ni mmoja kati ya watu maarufu ambao tunaweza sema hawana bahati katika mapenzi, tangu enzi za Wolper, akaja mzungu Sarah, mwigizaji Kajala kabla ya kuachana na kurudiana tena.

Katika mahojiano baada ya kuachana na Wolper 2017, Harmonize alisema kuwa alikuwa mjinga katika uhusiano huo kwani yeye ndiye alikuwa akifadhili maisha yake ya uchepukaji bila kujua.

“Nilipotembelea Marekani, yeye pia, kwa bahati nzuri alisafiri kwenda Burundi kikazi,” Harmonize alifunguka. Kule Burundi kuna mwanaume mmoja alimtembeza kwa gari aina ya Range Rover, nilipoona picha zao wakiwa pamoja, nikamuuliza, akasema ni mwenyeji wake ni kaka na hakuna kitu cha kufanya. Mwezi mmoja kabla, alikuwa ameenda China, na nilimpa Tsh30 milioni kama mtaji wa kuhifadhi nyumba yake ya mitindo," alisema Harmonize.

Baada ya kuachana naye, msanii huyo hakukaa mud asana mara akazama kwenye penzi zito na Sarah Michelloti, mwanadada kutoka Italia ambaye wengi wamekuwa wakisema kuwa ndiye alimpa sura mpya katika Sanaa ikiwemo kufanikisha kuvunja mkataba wake kule Wasafi na kuazna lebo yake ya Konde Gang.

Lakini hawa nao hawakukaa pamoja kwa muda kwani Michelloti alijikata kwa kusema kuwa msanii huyo alikuwa anamsaliti kimapenzi.

Baadae Harmonize alipokuwa kweney uhusiano na Kajala – baada ya kurudiana kwa mara ya pili mwaka 2022, Michelloti alirejea kwa kishindo, safari hii si kutaka kurudiana naye bali kutaka mgao wake katika mali ya msanii huyo, akidai kwamba ndiye alimfadhili pakubwa baada ya kudaiwa kufilisika alipovunja mkataba wake na lebo ya Diamond.

Na mzungumzo wa maisha ya kimapenzi ya Harmonize umekuwa hivo hivo hadi miezi michache iliyopita akafanya udhubutu wa kufanya wimbo wa kujiliwaza kwamba yuko singo tena.

Lakini je, unahisi msanii huyo ni bahati hana katika mduara wa mapenzi au ni ujinga na upuuzi wa kuzama kwenye mapenzi kwa haraka bila kujali mustakabali wa mahusiano hayo? Na je, unahisi anafaa kuingia kwenye uhusiano mpya au achukue muda mbali kidogo na kiazi moto cha mapenzi?

View Comments