In Summary

• Rapa huyo alizidi kumshukuru Zuchu kwa kumuiga.

• Katika kujibu kwa haraka, Stivo Simple Boy aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram na kushiriki upya video ya Zuchu akimuiga.

Stevo afurahia Zuchu kumuiga
Image: Instagram

Msanii Stevo Simple Boy ni mwenye furaha ya mbingu ya saba baada ya malkia wa Bongo Fleva Zuchu kufanya skit ya TikTok akiiga sauti ya msanii huyo.

Zuchu alipakia klipu hiyo akiiga sauti ya Stevo Simole Boy ambayo alikuwa akizungumzia kuhusu mpenzi wa zamani, akilenga mkuki wake kwenye kambi ya aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy kuwa hafai kumkaribia kabisa, na msanii huyo wa Kenya alipakia klipu hiyo akionesha furaha yake tele.

"Ma-ex wakae kando sahi nko na barafu wangu wa moyo. [Ananipea] mahaba, kunikanda ehh kuniandalia mamkuli," Zuchu alisema huku akimuiga Stivo Simple Boy.

Katika kujibu kwa haraka, Stivo Simple Boy aliingia kwenye akaunti yake ya Instagram na kushiriki upya video ya Zuchu akimuiga.

Rapa huyo alizidi kumshukuru Zuchu kwa kumuiga.

“Haya hata @officialzuchu ashasema ma ex wakae kando Habari iwafikie jamani wengine tuna barafu wetu wa moyo 😂😂😂❤️,” Stivo aliandika.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Stevo walimtaka kutumia fursa hiyo na kumuomba Zuchu mkono katika kushirikiana pamoja kufanya collabo.

“Stevo sasa usilalishe, tumia fursa hii kuomba collabo kwa mpenzi wa Diamond. Fom imejipa,” mmoja alimshauri.

 

View Comments