In Summary

• Mpaka sasa, zaidi ya maiti 39 imefukuliwa katika shamba la mchungaji Mackenzie huko Kilifi.

Mtangazaji Gidi Ogidi

Mtangazaji wa Radio Jambo Gidi Ogidi amekuwa mtu wa hivi punde kuweka kwenye mizani ya maoni mjadala kuhusu dini n viongozi wake, haswa kutokana na mchungaji Paul Mackenzie kutoka Kilifi kuwaamrisha waumini wa kanisa lake kujitesa njaa hadi kufa ili ‘kukutana na Mungu’.

Kulingana na Gidi, ni wakati sasa serikali inafaa kuwalinda watu wake kutokana na hulka za wahubiri wa aina hiyo ambao wanatumia uhuru wa kuabudu visivyo.

Gidi anahoji kwamba serikali inafaa kuwakamata wachungaji wote wanaojitapa kuwa wana uwzo na upako wa kipekee kaitka ulimwengu wa kiroho kuponya magonjwa na matatizo sugu, na kuwapeleka hospitalini kwa wagonjwa hao ili kuona kama kweli wana uwezo wa kutoa uponyaji.

“Serikali iwakusanye wachungaji wote wanaodai kuponya walemavu, vipofu n.k kisha kuwapeleka katika hospitali zote mmoja baada ya mwingine,” Gidi alisema.

Endapo wataweza kutamka miujiza yao na vipofu kuona, viwete kitembea na matatizo mengine kutatuliwa, wachungaji wa aina hiyo basi wapewe vyeti maalum kwa ajili ya kufanya kazi ya kueneza Neno, na ikiwa watafeli basin a wakachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwarubuni wananchi kwa jina la Yesu, Gidi alisema.

“Ikiwa miujiza yao itatenda, wanapaswa kupewa leseni maalum ya kitheolojia. Lakini kama sivyo wanapaswa kupigwa marufuku kutoka kwa shughuli zozote zinazohusiana na kanisa maisha yao yote,” Gidi alihisi.

Mpaka kufikia sasa, maafisa wa polisi wamefukua miili zidi ya 39 kutoka kwa shamba lenye ekari 800 la mchungaji Mackenzie lililopo Shakahola kaunti ya Kilifi, wengi wa waathiriwa wakitajwa kuwa watoto.

View Comments