In Summary

• Alimalizia akimtaka Kibe kama kweli maisha yake yanatia fora huko Marekani, ayaweke mitandaoni kwa wiki moja tu.

Akothee na Andrew Kibe wakabana koo.
Image: Facebook

Mjasiriamali na msanii Akothee hajafurahishwa na jinsi mwanablogu Andrew Kibe amekuwa akimshambulia kwa maneno tangu alipofunga harusi na mpenzi wake wa kutoka Uswizi, Denis Schweizer almaarufu Mr Omosh.

Jumanne Kibe alifanya video akiwalinganisha Akothee na Millicent Omanga katika weledi wao kwa maswala ya chumbani, jambo ambalo Akothee aliona ni kama kuwakosea wanawake heshima na kutoa tahadhari kali kwa mwanablogu huyo aliyeko Marekani.

“Sasa hii sio kuridhika bali ni kutoheshimu wanawake. Andrew Kibe kuwa makini kufukuza kiki kusije kukakusukuma jela. Hauko juu ya sheria kuamka tu na kupiga kelele, Sote tunaelewa kuwa umevunjika, una uchungu na ni mtu sumu, unaweza kuunda aina zote za maudhui. Lakini sitakuruhusu uende hadi hapa,” Akothee alimwambia.

Aidha, msanii huyo ambaye hajui kubakisha maneno ya akiba alimsuta vikali Kibe akisema kuwa anawakejeli wanawake wakati yeye mwenyewe hawezi hata kumtongoza nzi, huku pia akimwingilia vikali kuwa hana uwezo wa kumkidhi mwanamke maswala ya seksheni chemba.

“Wewe mwenye huwezi hata tongoza Nzi huna nguvu ya kiume ama pombe zilikumaliza kitaambo. Wewe ni mtu wa kushindwa katika maisha, kwa hiyo unaona maisha yako ndani ya mafanikio ya watu wengine. Unapotosha kizazi kipya na bidhaa yako yenye sumu,” Akothee alisema.

Alimalizia akimtaka Kibe kama kweli maisha yake yanatia fora huko Marekani, ayaweke mitandaoni kwa wiki moja tu ili watu waone na kama hatoweza basi awe tayari kurudishwa Kenya kujibu mashtaka ya kuwakejeli wanawake kila siku.

“Ikiwa unaendelea vizuri nchini Marekani unaweza kuandika maisha yako kwa wiki bila kugusa haiba. Unaweza kutuchapishia bili unazotunza huko US. Tutakurudisha kenya kujibu maswali yote unayouliza. Ni lazima uwajibike kwa matendo yako Nugu.”

View Comments