In Summary

• Madowo alianza kazi yake katika KTN akiwa na umri wa miaka 20, kama ripota chipukizi.

• Madowo katika taaluma ya kumeta pia amefanya kazi katika NTV na CNBC Africa.

Larry Madowo arejea kwa Ex wake, BBC
Image: Facebook

Mtangazaji maarufu wa CNN kutoka Kenya Larry Madowo anahoji kama kuna ubaya mtu ukiamua kurudi kwa mpenzi wake wa zamani japo kwa siku moja tu kisha kuendelea na maisha yako ya kawaida baadae.

Hii ni baada ya Madowo kurejela katika studio za shirika la habari la kimataifa kutoka Uingereza BBC, ikiwa ni miaka miwili tangu alipogura akipata kazi mpya katka shirika la habari kutoka Marekani, CNN.

“Je, ni kudanganya ikiwa mpenzi wako wa zamani anakurudisha kwa siku 1 na unakubali sasa hivi? Nilikuwa kwenye BBC kwa mara ya kwanza tangu niondoke miaka 2 iliyopita,” Madowo alidokeza.

Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba alirudi BBC kwa ajili ya kazi bali tu alitembelea studio hizo kama njia moja ya kukumbuka alikokuwa akifanya kazi zamani na kuchochea urafiki mzuri baina yake na aliyekuwa mwajiri wake.

Larry Madowo ni mmoja wa waandishi wa habari waliofanikiwa zaidi nchini Kenya ambaye anafanya kazi CNN kama mtangazaji wa African Voices Changemakers.

Mwanahabari huyo alijiunga na CNN kutoka BBC mnamo Mei 2021, ambapo alikuwa akifanya kazi kama Mwandishi wa Afrika kwa kampuni kubwa ya vyombo vya habari.

Madowo alianza kazi yake katika KTN akiwa na umri wa miaka 20, kama ripota chipukizi. Madowo katika taaluma ya kumeta pia amefanya kazi katika NTV na CNBC Africa.

View Comments