In Summary

• Atwoli alisema kuwa majukumu ambayo Kilobi anayafanya kwenye maisha yake ni yale ambayo mtu mwingine yeyote hangefanya.

• Atwoli alisema hangeweza kumtafuta msaidizi wa kumfanyia majukumu hayo kwani anaogopa kuibiwa.

Francis Atwoli na mkewe mdogo Mary Kilobi wakiwa ndani ya ndege
Image: Instagram

Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini Kenya, COTU, Francis Atwoli aliwaacha wakenya wakiwa na kicheko kirefu wakati wa kutoa hotuba yake kuashimisha siku ya wafanyikazi Mei mosi jijini Nairobi.

Mzee Atwoli mwenye umri wa miaka 73 kwa mara ya kwanza alizungumzia majukumu ya mke wake Mwanahabari Mary Kilobi mwenye umri wa miaka 38.

Atwoli alisema kuwa yeye ni mzee sasa na hawezi fanya mengi na kusema kuwa sababu kuu yake kumuoa Kilobi ilikuwa ni kutotaka kuandika mtu kazi ambaye hamjui nap engine angekuja kumshuru ikiwemo kumuibia mali yake.

Atwoli alisema kuwa Kilobi anafanya kazi kubwa katika maisha yake ikiwemo kuangalia mavazi yake, kumkumbusha muda wa kumeza dawa miongoni mwa majukumu mengine ambayo mtu mwingine wa nje hangeweza kuyafanya.

“Mimi sasa ni mzee hata kama mnaona mke wangu hapa ni kijana. Mary Kilobi kazi yake ni kuangalia soksi yangu ninayovaa kama iko sawa, kunikumbusha kuwa muda wa kumeza dawa umefika, nikitaka kwenda ulaya ananiambia ndege ni saa ngapi…” Atwoli alisema.

Katibu huyo mwenye ucheshi wa aina yake pia aligusia kwamba Kilobi humkumbusha kuhusu mavazi aliyovaa jana na kumkumbusha asiyarudie, kumuelekeza njia ya kupitia miongoni mwa kazi zingine ambazo hufanywa na msaidizi.

“Hili begi umebeba ni la mwaka jana, geti unafaa kupitia ni hili … hiyo ndio kazi ya Mke wangu Mary Kilobi,” Atwoli alisema.

Kando na kuzungumzia majukumu na sababu za kumuoa Kilobi kama mke wake, pia aligusia siasa na kukumbuka jinsi alivyokuwa katika mstari wa mbele kumpigia debe kinara wa Azimio Raila Odinga bila mafanikio.

Atwoli alisema kuwa kwa kipindi kimoja walikutana na aliyekuwa mbunge wa Starehe Maina Kamanda ambaye aliwapa onyo la mapema kuwa aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta hangemfaidi Odinga kitu chochote katika mbio zake za kumrithi katika ikulu ya Nairobi.

View Comments