In Summary

• “Sawa acha tujaribu hi tena, mbona niko singo?” Jazzy aliandika kwenye video hiyo, "ni kwa sabau sitaki kujukumika,"

Harmonize mawinguni Don Jazzy akishiriki Single Again
Image: Instagram

Baada ya msanii maarufu Afrika, Davido na mkewe kuonesha wazi wazi mapenzi yao kwa wimbo wa Single Again kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa lebo ya Konde Music Worldwide, mkurugenzi mkuu mtendaji wa lebo maarufu ya muziki Marvin Records, Don Jazzy naye pia ameupa shafu wimbo huo.

Jazzy kupitia ukurasa wake wa TikTok alipakia video mbili akiwa anaimba wimbo huo wa Harmonize kama njia moja ya kuonesha kuukubali kupita maelezo.

Don Jazzy alipakia wimbo huo akitania kwamba yuko singo baada ya msanii Rihanna ambaye alitajwa kuwa anampenda sana kuolewa na rapper Asap Rocky.

“Sawa acha tujaribu hi tena, mbona niko singo?” Jazzy aliandika kwenye video hiyo, "ni kwa sabau sitaki kujukumika,"

 Hata hivyo, akiwa na furaha kubwa, Harmonize alishiriki kipande hicho cha video kwenye Instagram yake akisema kuwa kumepambazuka upande wake kwani CEO wa lebo kubwa Zaidi duniani aliweza kuufikia wimbo wake na kuupenda miongoni mwa mamilioni ya ngoma nzuri ambazo zipo pale nje kwenye soko.

Konde alimliwaza Jazzy akimwambia kuwa atamtafutia Rihanna mwingine kutoka Tanzania ili kuhakikisha kwamba hatokuwa singo tena.

“Mabibi na mabwana bosi mkubwa Don Jazzy hayuko tayari kujukumika baada ya Asap Rocky kumchukua Rihanna. Usiwe na shaka baba Jazzy, nitahakikisha umepata Rihanna mwingine kutoka Tanzania ili usiwe singo tena,” Harmonize aliandika.

Baadhi ya wachambuzi wa tasnia ya burudani walihisi kwamba hii ndio fursa ya kipekee ambayo imemtokea Harmonize machoni na hafai kuiacha ipotee kwani kupitia kwa Jazzy, kuna uwezo mkubwa sana wa kumpata msanii mkubwa wa Marvin Records atakayedandia kwenye remix ya Single Again na kuifanya kuwa kubwa kuliko.

View Comments