In Summary

• Njoroge kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa mara ya kwanza alifichua kuwa miaka michache nyuma alibeba ujauzito wa mapacha ambao kwa bahati mbaya uliharibika.

Pauline Njoroge adhibitisha kuharibikiwa na ujauzito
Image: Facebook

Jumapili Mei 14 ilikuwa siku spesheli kwa kina mama kote duniani ambapo watu walijumuiika kuwasherehekea viumbe hao katika siku hiyo iliyotengwa mahsusi kumsherehekea kila mwanamke ambaye ni mama.

Wengi walijumuika mitandaoni wakisherehekea wavyele wao wa kike kwa kuwazaa na kuwapa malezo bora huku kina mama wengine wkijisherehekea katika njia sawia.

Hata hivyo, kuna wengine waliosherehekea kwa jumbe zenye ukakasi na za kubutua mioyo; hawa wakiwa ni wale waliopoteza wazazi wao wa kike na pia kina mama waliopoteza watoto wao ambao wangewafanya kuitwa mama.

Mmoja wa waliosherehekea kwa njia hii ni mwanablogu wa masuala ya kisiasa Pauline Njoroge.

Njoroge kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa mara ya kwanza alifichua kuwa miaka michache nyuma alibeba ujauzito wa mapacha ambao kwa bahati mbaya uliharibika.

Bila shaka kuharibika kwa ujauzito ni jambo ambalo hakuna mama yeyote anaweza kulihimili kwani huja na uchungu uliopitiliza ambao hauwezi kupimika kwa mizani ya dunia hii wala kuonekana kwa darubini za macho ya kibinadamu.

Njoroge, kama mwanamke yeyote aliumia. Alipitia wakati mgumu kuona vijusi wake wakipotea mazima katika matone ya damu, lakini ndio hivo hakuwa na jinsi kwani yalishamwagika!

“Kwa muda wa miezi kadhaa nilikuwa nimechanganyikiwa kihisia-moyo na hakuna kitu kingeweza kunifariji. Nililia mara milioni na machozi yakawa chakula changu cha kila siku. Huku nje niliweka uso mkali kwa sababu wakati mwingine sisi wanawake na viongozi, hatuna anasa ya kusambaratika hadharani bila kujali kinachotokea ndani,” Njoroge alisema kwa uchungu.

Wakati asilimia kubwa ya wafuasi wake walionekana kumpa pole na kumtamkia maneno ya kumhimiza, kunao wengine waliona kivuno katika kumshambulia.

Mwanamume mmoja alionekana kuandika maneno yenye makali ncha kuwili, akimpiga mateke wakati tayari Njoroge anariya sakafuni.

Kip Korir, kama alivyojiita mwanamume huyo aliona raha kuchomeka msumari wa moto kwenye donda la Njoroge.

Mwanamume huyo alimtukana Njoroge kuwa hali yake ya kupoteza vujusi wake ilichangiwa na kile alichokiita matumizi ya mpango wa uzazi akiwa mdogo lakini pia maneno mengine yenye ukakasi ambayo hayawezi kutoka mdomoni mwa mtu mwenye zake razini kichwani.

 

View Comments