In Summary

• “Vaa vizuri kaka kama hao watu wengine, unakaa kama mlinzi,” jamaa huyo aliwandikia Olunga.

Mara nyingi watu hupenda kuwazengua wenzao maarufu mitandaoni kwa maoni na kauli za kejeli, na wengi hutamba kwa kuandika pumba kwenye akaunti za watu na kuondoka nayo.

Baadhi ya watu maarufu hujitoa mhanga na kujibu mipigo, na aghalabu majibu yao huwa ya kukalifisha mno.

Ndio mtindo ambao mchezaji wa kimataifa ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa Harambee Stars Michael Olunga ameukumbatia.

Olunga alimpiga kumbo jamaa mmoja kwenye mtandao wa Facevook aliyekejeli fasheni yake aksiema kuwa mavazi yake ni kama ya walinzi ambao wanafanya kazi nchini Qatar – taifa ambalo mchezaji huyo anasakata kabumbu.

Olunga alipakia picha akiwa amesimama kando na watu wengi waliokuwa wakijishughulisha na mambo yao mbele ya jingo la kihistoria akiwa amevalia koti na jamaa huyo akaidakia akimsuta kuwa hakuwa amevaa vizuri kama watu wengine walioonekana kwenye picha hiyo.

“Vaa vizuri kaka kama hao watu wengine, unakaa kama mlinzi,” jamaa huyo aliwandikia Olunga.

Olunga hata hivyo alishindwa kumeza hili lililokaa dharau Zaidi ya ushauri na kuichukua picha ya utambulisho na mwanamume yule na kuipakia akimjibu kuwa angependeza sana iwapo angempa hiyo tisheti yake.

Nisaidie hii polo nivae inaweza nisaidia,” Olunga alimjibu shombo.

Olunga aliwajibu vikali waliokita kambi kwenye chapisho hilo lake wakisema kuwa alikuwa hajapendeza kabisa katika mavazi yake.

“Bro hata wazungu wanashangaa na wewe, unakaa tu kienyeji na hiyo toolbox yako,” mwingine alisema.

View Comments