MAPENZI YENYE UTANI
Zuchu aeleza kwa nini hawezi kumuacha Diamond licha ya kum'cheat na Fantana
Huwezi cheat mbele ya macho yangu nikakusamehe, hilo haliwezi tokea," Zuchu alisema.
•Zuchu alieleza kuwa kusalitiwa kimapenzi si hoja kwake bali hoja ni kumletea mwanamke mwingine katika nyumba yake.
•Siku za hivi majuzi, Diamond amedaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Fantana.
Mwimbaji Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu ameeleza kwa nini hawawezi akamuacha Diamond Platnumz hata akimsaliti kimapenzi.
Zuchu alizungumzia hili baada ya video ya Diamond akibusu na mwimbaji wa kutoka Ghana Francine Koffie maarufu Fantana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Katika video hiyo Diamond alikiri kwamba hajawahi kupata busu jingine kama hilo alilopata kwa Fantana.
Nyota huyo ambaye kibao chake cha ‘Sukari’ kilivuma sana, alieleza kuwa kusalitiwa kimapenzi si hoja bali hoja ni kumletea mwanamke mwingine katika nyumba yake.
“Kucheat inategemea. Huwezi cheat mbele ya macho yangu nikakusamehe, hilo haliwezi tokea. Lakini ati umecheat zako huko makampepaka, nyumbani tukiwa wawili hehehe. Wewe utakaa huko na baby wako tutakutana nyumbani,” Zuchu alisikika akisema katika video iliyosambaa mitandaoni.
Diamond alidaiwa kuanza kusuhubiana na Zuchu mwaka wa 2021. Mwezi Februari mwaka huu aliweka bayana katika mitandao kwamba uhusiano wake na msanii huyo wake wameutilia kikomo na kurejelea uhusiano wa kindugu.
Siku za hivi majuzi, bosi huyo wa WCB amedaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Fantana, hali ambayo imeonekana kumpa Zuchu sintofahamu katika mapenzi.
Katika Video nyingine, Zuchu alisema kwamba Diamond humpa kile ambacho anahitaji, akiongeza kwamba bosi huyo anamfuata kwa sababu ya umbo lake.“Simba anasema ndio kila ninalomwambia, bwana anasema ndio kila ninalomwambia. Moyo humuenda mbio jina akilisikia. Hajafwata makalio amekipenda kifua,” Zuchu aliimba.