In Summary

• Msanii huyo wa ‘Kioo’ alipakia picha ikimuonesha akiwa katika riziki ya upambanaji wa kuuza mkaa, huku akiwa amechaka.

Anjella aonekana akiuza makaa, mapambano ya kuepuka ufukara.
Image: Instagam

Msanii aliyekuwa amesajiliwa kwenye lebo ya Harmonize, Konde Music Worldwide, Anjella amevunja kimya chake cha muda mrefu katika muziki, miezi kadhaa baada ya kuondoka katika lebo hiyo kwa ukakasi mwingi.

Anjella kupitia ukurasa wake wa Instagram alidokeza kurejea tena kwenye muziki na dude jipya na kupakia picha inayokisiwa kuwa kutoka moja ya onyesho la maigizo ya video ya ngoma yake mpya inayotarajiwa kuwa na maudhui ya upambanaji.

Anjella alisema kuwa alizaliwa kufanya muziki na katu hatoweza kumudu kufa moyo kwani muziki ni yeye na yeye ni muziki, huku akitangaza ujuo wake mpya na kufutilia mbali uvumi kwamba alizama baada ya kuachiliwa na Harmonize.

Mziki kwangu mimi ulikuwa ndoto na sikuitimiza kwa kulala napitia nyingi changamoto yote kuukimbia ufukara😔bado sijakata tamaa,” Anjella aliandika.

Msanii huyo wa ‘Kioo’ alipakia picha ikimuonesha akiwa katika riziki ya upambanaji wa kuuza mkaa, huku akiwa amechakaa na mbele yako akionekana mvulana mdogo anayekisiwa kuwa mteja wa kununua mkaa akimnyooshea noti kwa ajili ya kupewa mkaa.

Anjella tangu aondoke Konde Gang amekuwa adimu kuonekana katika kutoa kazi zake mweneywe za muziki na kwa muda wote amekuwa akionekana kushiriki katika kazi za wasanii wengine.

View Comments