In Summary

• Shakila alipewa marufuku hiyo baada ya kuzidisha kukaa kwake kwenye taifa ya Uturuki kwa miezi miwili.

• Shakila ambaye amekuwa Uturuki kwa muda sasa ambapo alikuwa ameenda kumtembelea mpenzi wake alikuwa akirejea Kenya baada ya kukaa huko kwa zaidi ya miezi minne.

Mwanasoshialaiti Shakila.
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshialaiti Shakila Tiffany anayefahamika kama Shakila amepigwa marufuku ya miezi miwili asifike Uturuki.

Shakila aliwaarifu mashabiki wake kuwa sasa alihitajika kulipa kima cha dolla 45 ambaye ni sawa na shilingi 62,000 ya Kenya.

‘’Na ni hivo ndivyo nimepoteza dolla 450 na marufuku ya kutofika Uturuki  miezi miwili kwa sababu ya kukaa huku miezi miwili zaidi.’’ Ilisoma tarifa hio.

Shakila alipewa marufuku hiyo baada ya kuzidisha kukaa kwake kwenye taifa la Uturuki kwa miezi miwili.

Shakila ambaye amekuwa Uturuki kwa muda sasa ambapo alikuwa ameenda kumtembelea mpenzi wake alikuwa akirejea Kenya baada ya kukaa huko kwa zaidi ya miezi minne.

Aidha Shakila hakufichua jina wala sura ya mpenzi wake aliyekuwa akikaa naye Uturuki.

Shakila awali alikuwa amesema kuwa hawezi akajihusisha katika mahusiano na mwanume kutoka Kenya.

Siwezi kuchumbiana na Mkenya kamwe. Mimi si Mkenya kwa hivyo nina haki ya kufanya hivyo."

Kulingana naye angependelea kuchumbiana na wanaume wa Nigeria, ambao aliwasifu kwa ukarimu wao.

"Wanigeria ndio watu watamu zaidi unaoweza kukutana nao, wanakupa pesa na kukutendea mema.

View Comments