In Summary

• Kwenye kionjo hicho, Darassa aliandika kwamba ndio yuko kwenye stoo akitoa zana zake tayari kwa maangaamizi.

• “NIKO STOO NAFUTA FUTA SILAHA ZANGU ZA MAANGAMIZI,” Darassa alisema kweney video hiyo.

Diamond amvika kiremba cha ufalme Darassa.
Image: Instagram

Diamond Platnumz kwa mara nyingine amejikuta kwenye gumzo mitandaoni baada ya kumvika rasmi msanii wa rap Darassa kuwa ndiye mfalme wa mtindo wa miziki ya kufoka nchini Tanzania.

Hii ni baada ya msanii Darassa kuchapisha kionjo cha video ya ngoma yake mpya kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa na mtindo wa Drill.

Ikumbukwe kwa kipindi cha kama mwaka mmoja hivi, msanii huyo alikaa kimya bila kutoa muziki wowote lakini miezi michache iliyopita alirejea kwa kuachia ngoma tatu kwa mkupuo.

Kwenye kionjo hicho, Darassa aliandika kwamba ndio yuko kwenye stoo akitoa zana zake tayari kwa maangaamizi.

NIKO STOO NAFUTA FUTA SILAHA ZANGU ZA MAANGAMIZI,” Darassa alisema kweney video hiyo.

Hata hivyo, gumzo kubwa lilichipuka baada ya Msanii Diamond kupitia kipengele cha kutoa maoni kumpa maua yake Darassa huku akimtambua kama mfalme wa rap nchini Tanzania.

Darassa alimshukuru Diamond kwa kumvika kiremba cha ufalme wa Rap huku pia akimpongeza kuwa yeye ni madini mwenzake ambayo imeitambua madini nyingine.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita wakati taifa hilo lilikuwa linaadhimisha miaka 10 tangu kifo cha msanii mkali wa rap Albert Ngwair, wengi waling’aka kwamba tangu kifo chake hakuna msanii mwingine wa rap amekuwa na udhubutu wa kuziba pengo lake licha ya kwamba kuna utitiri mwingi wa wasanii wa mtindo huo.

Mpaka kifo chake mwaka 2013, Ngwair alikuwa ameachia ngoma nyingi za rap na mashabiki wengi wanahisi kwamba hakuna msanii mwingine ambaye ametokea kuwakatisha kiu chao cha miziki ya rap.

View Comments