In Summary

• "Sasa ninawaomba viongozi wetu wa Kenya, leo hii si punda, ni gari,” Nabii Benjamin alisema.

Mkewe Yesu wa Tongaren ni aomba gari.
Image: Screengrab

Nabii Benjamin, mke wa Yesu wa Tongaren ametoa wito na ombi kwa wahisani wema kumpa mumewe zawadi ya gari ili kurahisisha kazi ya kueneza injili ya babake, Mungu.

Katika video ya TikTok ambayo haijulikani ni lini wanafamilia hao walikuwa wanazungumza na wanablogu na wanahabari alisema kuwa Yesu anahitaji gari kutoka kwa wahisani wema au hata viongozi wa serikali.

“Jambo ambalo nimekuwa nalo kuwaambia viongozi wetu wa Kenya, ukisoma katika maandiko matakatifu Yesu alikuwa anatembea kwa punda. Na sasa hivi Yesu hawezi toka hapa hata akafika hapo tu kwa lami. Sasa ninawaomba viongozi wetu wa Kenya, leo hii si punda, ni gari,” Nabii Benjamin alisema.

Alitoa wito kwa wale wanaotaka huduma kuwa wakitaka Yesu awafikie kwa haraka basi wanafaa kumpa gari ili kumrahisishia usafiri.

“Sasa leteni gari mkitaka Yesu awafikie kwa haraka. Mtakuwa mmesaidia sana kwa sababu punda siku hizi hata hawako. Mungu alibadilisha siku hizi mnasema ni dijitali na hakuwezi kuwa na usafiri wa punda. Hata pikipiki yenyewe Yesu hana,” Nabii Benjamin alisema.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba Yesu hafai kupewa pikipiki na kusisitiza umuhimu wa gari kwa sababu katika pikipiki watu watakuwa wanamzingira Yesu wakimuimbia na hivyo kutatiza kuendeshwa kwake.

Yesu wa Tongaren anazidi kuwa gumzo la mitandaoni haswa baada ya kufika mbele ya polisi kwa usaili na kuishia kuwekwa ndani kwa kile alikuwa anatuhumiwa kuwa ni kutoa mafunzo ya kupotosha kwa waumini wake.

Hata hivyo baada ya siku nne kwenye seli, Yesu aliachiliwa huru bila mashtaka yoyote na ameendelea na huduma yake katika kaunti ya Bungoma.

View Comments