In Summary

• Wawili hao waliachana wiki chache zilizopita baada ya wawili hao kwenda kununua ya rinda la harusi.Hii iliashiria kuwa uhusiano wao ulielekea pazuri.

• Mzee huyo pia alikiri kuwa bado alikuwa anampenda binti huyo na ikiwa Manzi wa Kibera angependa warudiane ingekuwa sawa

Manzi wa Kibera na mpenzi wake wa zamani.
Image: INSTAGRAM

Mpenzi wa hivi majuzi wa Sheriffa Wambui almraafu Manzi wa Kibera alimsihi binti huyo kumregeshea hati miliki ya shamba lake.

Katika mahojiano na Nicholas Kioko, mzee huyo alisema alimpa hati hiyo ili aitunze huku wakipanga kujenga nyumba na kuanzisha familia pamoja.

Mzee huyo pia alikiri kuwa bado alikuwa anampenda binti huyo na ikiwa Manzi wa Kibera angependa warudiane ingekuwa sawa naye ila kama alihisi hawawezi kurudia mahusiano yao basi amrudishia hati miliki yake.

"Akileta hiyo na aniambie tuko pamoja nitakua sawa. Na yeye anipende kama vile nilikua nampenda mbeleni tukimaliza hiyo tupange harusi," aliongeza.

Wawili hao waliachana wiki chache zilizopita baada ya wawili hao kwenda kununua ya rinda la harusi.Hii iliashiria kuwa uhusiano wao ulielekea pazuri.

Katika majibu yake, Manzi wa Kibera alisema: "X wako akipiga simu unadhani wanataka mrudi kuchumbiana. Sikujua alikuwa akipiga simu kuhusu hati yake ya umiliki bila shaka nitairudisha."

Kulingana na mwanasosholaiti huyo anayeishi Kibera, baada ya kukejeliwa mitandaoni alilazimika kuachana na mzee huyo.  

Alisema alishindwa kuvumilia matusi na shutuma alizopata kwa kuchumbiana na mwanaume ambaye anamzidi umri kwa zaidi ya miaka 30 .

View Comments