In Summary

• Fahyvanny na Rayvanny walirudiana miezi michache iliyopita baada ya kila mmoja kujishughulisha na hamsini za kwake kwa kipindi cha miaka kama mitatu hivi.

Fahyma ajitetea kwa kuwa mfupi, asema wanawake warefu ni sanamu.
Image: Instagram

Mrembo wa msanii Rayvanny, Fahyma amekiri kwamba yeye ni mfupi sana ila akatetea watu haswa warembo wenye kimo cha mbilikimo.

Fahyvanny alikuwa anamjibu mrembo mmoja ambaye alisema kuwa yeye ni mfupi, kitu ambacho mwanamke huyo alikiita kuwa ndio doa pekee kwa mwili wa Fahyvanny ila katika sekta zingine ako vizuri na amebarikiwa.

“Tatizo ufupi, kila kitu unacho dada,” mrembo huyo kwa jina Abby the Bossy alisema.

Kimjibu, Fahyma alisema kuwa wala hajawahi babaishwa kuhusu urefu wake huku akisema kuwa mrembo huyo laity angalifanya utafiti wake vizuri kuhusu wanawake wafupi kabla ya kumwambia kuwa ufupi ni tatizo.

Alisema kuwa duniani kote wanawake wafupi ndio kusema huku akiwasusa walewarefu kuwa ni wazuri kwa ajili ya maonyesho tu na wakati mwingine wanachukuliwa kama sanamu.

“Urefu wa nini mimi. Kwanza wewe fuatilia vizuri warembo wafupi duniani ndio wazuri na ndio tunatesa na kusumbua sana,” Fahyma alisema.

“Hao warefu ni kwa ajili ya maonesho tu kama sanamu,” Aliongeza.

Fahyvanny na Rayvanny walirudiana miezi michache iliyopita baada ya kila mmoja kujishughulisha na hamsini za kwake kwa kipindi cha miaka kama mitatu hivi.

Wawili hao waliachana mwaka 2019 na walikuwa na mtoto mmoja wa kiume, Jayden.

View Comments