In Summary

• Shakur aliuawa mwaka wa 1996 akiwa na umri wa miaka 25 katika shambulio la gari huko Las Vegas ambalo halijawahi kutatuliwa.

• Moja ya sifa maarufu za Tupac ni pamoja na wimbo "Dear Mama," ambao uliwekwa wakfu kwa mama yake, Afeni Shakur.

Tuzo ya heshima za baada ya kifo kwa msanii Tupac Shakur aliyefariki miaka 27 iliyopita.
Image: Holywood Walk of Fane//Facebook

Rapa, mwanaharakati na mwigizaji aliyeshinda tuzo, Tupac Shakur alipokea nyota baada ya kifo chake, maarufu Posthumous kwa kimombo,  Jumatano kwenye Hollywood Walk of Fame, ambapo dada yake na wasanii wenzake walizungumza juu ya urithi wa mwanamuziki huyo kote ulimwenguni.

"Tupac alijua kabisa kwamba alikusudiwa kila wakati kwa kitu kizuri," dadake Sekyiwa Shakur alisema katikati ya umati wa watu karibu 100. “Kama dada yake mdogo, nilipata fursa ya kutazama ukuu huo ukitendeka.”

Shakur aliibuka kutoka utoto wa umaskini huko katika mitaa duni ya Harlem huko Marekani na kuwa mmoja wa wasanii wa muziki wanaouzwa zaidi na rekodi zaidi ya milioni 75 zilizouzwa duniani kote.

"Tangu mara ya kwanza alipokanyaga jukwaa la ukumbi wa michezo wa Apollo akiwa na umri wa miaka 13, kabla ya mtu yeyote kutambua jina lake, alijua alikuwa na ndoto ya kuwa na heshima hapa kwenye Walk of Fame," alisema.

Shakur aliuawa mwaka wa 1996 akiwa na umri wa miaka 25 katika shambulio la gari huko Las Vegas ambalo halijawahi kutatuliwa.

Washiriki wenzake wa kundi la muziki la marehemu rapper Outlawz, Malcom Greenidge, anayejulikana kwa jina lake la kisanii, E.D.I. Mean, na nguli wa hip-hop David Marvin, anayejulikana kama DJ Quik, pia walihudhuria sherehe hiyo.

Moja ya sifa maarufu za Tupac ni pamoja na wimbo "Dear Mama," ambao uliwekwa wakfu kwa mama yake, Afeni Shakur.

View Comments