In Summary

• “Tuna waundaji wa maudhui wanyoofu kama vile mvulana anayeiga Riggy G, ambaye anaweza kuwa msukumo wa kweli kwa mvulana." - Njohi alisema.

Kinuthi akiwa kwenye ikulu kwa uzinduzi wa Talanta Hela.
Image: Instagram

Ijumaa kulikuwa na uzinduzi rasmi wa mradi wa Talanta Hela katika ikulu ya Nairobi ambapo waziri wa michezo na maswala ya vijana Ababu Namwamba aliwaalika wanablogu na wakuza maudhui ainati kuhudhuria mradi huo.

Mradi wa Talanta Hela unalenga kuwanufaisha vijana na haswa wale wenye talanta mbalimbali kutoka uigizaji, Sanaa, uimbaji na michezo kupata hela kutokana na vipaji vyao.

Hata hivyo, si wanablogu au wakuza maudhui wote walioalikwa au kuhudhuria na wengine ambao walihudhuria wamezua mjadala mkali mitandaoni.

Kwa mfano, sehemu ya watu mitandaoni walihoji kwa nini serikali ambayo imekuwa ikisema ina maadili ya kiafirika na kidini, mbona walimualika mwanablogu Kelvin Kinuthia ambaye skits zake huwa anazifanya akiwa amevalia mavazi ya kike hali ya kuwa yeye ni mwanaume.

Kinuthia aliwasili ikulu akiwa amevalia kawaida kama mwanamke katika vazi la rangi nyekundu na hilo lilionekana kugawanya wengi.

Mwanablogu maarufu katika mtandao wa Facebook, Council Njohi alikashifu hatua ya serikali kumwalika Kinuthia hali ya kuwa jinsi ya uvaaji wake haina kiashiria chochote cha heshima kwa mila na tamaduni za kiafrika na kuwaacha nje baadhi ya wakuza maudhui ambao skits zao ni za kimaadii.

“Tuna waundaji wa maudhui wanyoofu kama vile mvulana anayeiga Riggy G, ambaye anaweza kuwa msukumo wa kweli kwa mvulana. Hata hivyo kumweka Kinuthia kama kielelezo cha ubunifu na kumwalika Ikulu akiwa amevalia kama mwanamke ni kinyume na roho ya "Sisi ni Waafrika na Afrika ni Biashara Yetu." ... Hatupaswi kamwe kuacha matarajio yetu ya kitamaduni,” Njohi alisema.

 

View Comments